Pata taarifa kuu
IRAQ

Wapiganaji zaidi kuingia kwenye mji wa Fallujah

Muungano wa wanajeshi wa Iraq ambao unaundwa kwa sehemu kubwa na wapiganaji wanaoungwa mkono na utawala wa Tehran, umesema uko tayari kutuma wanajeshi zaidi kwenye mji wa Fallujah ikiwa jitihada za kuuchukua mji huo zitaenda taratibu. 

Wapiganaji wanaopigana sambamba na vikosi vya Serikali ya Iraq wakiendeleza mashambulizi kulenga mji wa Fallujah
Wapiganaji wanaopigana sambamba na vikosi vya Serikali ya Iraq wakiendeleza mashambulizi kulenga mji wa Fallujah REUTERS/Alaa Al-Marjani
Matangazo ya kibiashara

Majeshi ya Iraq yalianzisha operesheni maalimu ya kuuchukua mji huo toka kwenye mikono ya wapiganaji wa Islamic State, May 22, mji ambao uko umbali wa kilometa 50 magharibi mwa mji mkuu Baghdad.

Wapiganaji wa kundi la The Hashed al-Shaabi toka awali limekuwa likishiriki kwenye operesheni za kujaribu kuuchukua mji wa Fallujah, lakini wakajikita kuchukua miji ya pembezoni ambako sasa wanafanya msako wa nyumba kwa nyumba.

Waziri mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, ameeleza wazi msimamo wake kuwa wapiganaji wa Hashed hawataruhusiwa kuingia kwenye mji wa Fallujah, akihofia kutokea kwa mapigano ya kikabila na hasa kwa jamii ya kusini.

Hata hivyo kamanda wa kundi hilo aliyefahamika kwa jina la Abu Mahdi al-Mohandis, amesema kundi lake halitasita kuingia kwenye mji huo ikiwa mapigano yataendelea bila Islamic State kudhibitiwa.

"Sisi ni washirika katika harakati za ukombozi, kazi yetu bado haijaisha," alisema waziri mkuu wa Iraq alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Baghdad.

"Tumemaliza kazi tuliyokuwa tumetumwa ambayo ilikuwa ni kuuzingira mji wa Fallujah huku harakati za ukombozi zilikuwa zimekabidhiwa kwa makundi mengine," ameongeza waziri mkuu.

Kundi la Hashed limedai kuwa kwa sehemu kubwa makundi mengine ya wapiganaji yamefanikiwa kuuzingira mji wa Fallujah, na kwamba zaidi ya wapiganaji elfu 2 na 500 wa Islamic State wamenaswa.

Wakisaidiwa na mashambulizi ya anga, kikosi maalumu cha Iraq cha kupambana na ugaidi, kwa juma moja lililopita kimekuwa kikijaribu kuingia katikati ya mji wa Fallujah, lakini wamejikuta wakipunguzwa kasi na upunzani toka kwa wapiganaji wa islamic State.

Mashirika ya misaada yanahofia kuhusu hali mbaya ya kibinadamu kwenye mji wa Fallujah, ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya raia elfu 50 wamenaswa kwenye mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.