Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan: zaidi ya watu 73 wafariki katika ajali ya barabarani

Watu wasiopungua 73 wamepoteza maisha Jumapili hii katika ajali ya mabasi mawili yaliyogongana na lori lililokua limebeba mafuta na kusababisha mlipuko mkubwa kwenye barabara, mashariki mwa Afghanistan, Wizara ya Afya ya afghanistan imetangaza.

Gari la wagonjwa likimsafirisha katika hospiali ya Ghazni mtu huyu aliejeruhiwa katika ajali ya mabasi mawili yaliyogongana na lori la mafuta kwenye barabara kuu inayotokea Kabul kuingia Kandahar, afghanistan Mei 8, 2016.
Gari la wagonjwa likimsafirisha katika hospiali ya Ghazni mtu huyu aliejeruhiwa katika ajali ya mabasi mawili yaliyogongana na lori la mafuta kwenye barabara kuu inayotokea Kabul kuingia Kandahar, afghanistan Mei 8, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Wahanga wengi wameteketea kwa moto katika ajali hii mbaya kabisa kuwahi kutoka nchini humo kwa miaka kadhaa.

Ajali hii imesababisha shughuli kwenye barabara hiyo inayotokea katika mji wa Kabul kuelekea katika mkoa wa Kandahar kusimama kwa masaa kadhaa kutokana na moshi mweusi uliokatiza usafiri, msemaji wa Wizara ya Afya, Ismail Kawoosi amesema. Watu wengine kadhaa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali za mjini Kandahar na Ghazni wakiwa katika hali mbaya. Inaarifiwa kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Eneo ambapo ajali hii ya kutisha imetokea ni moja ya mikoa ya Afghanistan inayoathirika zaidi na uasi wa Taliban. Wengi mwa madereva wa mabasi huendesha magari yao kwa umakini na kwa mwendo wa kasi kwenye barabara hii inayopita katika maeneo hatari, ili kuepuka mashambulizi ya waasi wa kundi laTaliban.

"Dereva wetu ana kosa, amekuwa akiendesha gari kama mwendawazimu," Esmatullah, mmoja miongoni mwa abiria wachache waliopata majeraha madogo katika ajali hii hatari amesema.

"Madereva wengi wanaotumia barabara hii kuu hujihusisha na madawa ya kulevya, wanatumia hashish, hiyo inajulikana. Na wengi wanajikuta wanashindwa kudhibiti magari wanayoendesha, "Esmatullah ameongeza.

Ajali mbaya zinatokea mara nyingi kwenye barabara mbalimbali nchini Afghanistan. Mwezi Mei 2005, watu kumi na nane walipoteza maisha wakati basi ndogo waliokuwemo lilipopinduka kwenye barabara ya mkoa wa Badghis, kaskazini magharibi mwa Afghanistan. Mwezi Aprili 2013, watu 45 walipoteza maisha katika ajali ya basi iliyogongana na lori lililokua likibeba mafuta kusini mwa mkoa wa Kandahar.

Mwezi Novemba, Benki ya Dunia ilitenga Dola milioni 250 ili kukarabati barabara zinazopita katika milima ya Hindu Kush, barabara muhimu hasa kwa biashara na ambazo mara nyingi zinafungwa kutokana na theluji wakati wa baridi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.