Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-USHIRIKIANO

Israel yataka kufungua upya eneo la mpaka wa Gaza

Waziri wa ulinzi wa Israel Moshe Yaalon ametangaza Jumatatu hii kwamba hivi karibuni bidhaa zitaruhisiwa kupita kwenye moja ya maeneo makuu yanayounganisha Israel na Gaza, lililofungwa kwa takriban miaka 8.

Malori yabeba mifuko ya saruji yanaingia katika Ukanda wa Gaza yakipitia katika eneo la Kerem Shalom, kusini mwa Gaza, Oktoba 14, 2014.
Malori yabeba mifuko ya saruji yanaingia katika Ukanda wa Gaza yakipitia katika eneo la Kerem Shalom, kusini mwa Gaza, Oktoba 14, 2014. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo hakutoa tarehe halisi kwa kufungua upya barabara ya Erez, kaskazini mwa Palestina, akionya tu kwamba "haitokua kesho au kesho kutwa".

"Ni maslahi yetu kuwa kiasi kikubwa cha magari yanayobeba chakula kuendelea kupita Gaza. Ni maslahi yetu wakazi wa Gaza waishi kwa kwa furaha, amani na upendo. Ni katika hali ya kuheshimu haki za binadamu na ni moja ya kuleta utulivu, licha ya hali ya usalam kuendelea kuzorota, " msemaji wa Bw Yaalon amesema katika taarifa yake.

Yaalon pia ameeleza haja ya kupunguza msongamano katika barabara ya Kerem Shalom, eneo mja tu la kupitisha bidhaa kati ya Israel na Ukanda wa Gaza, kusini mwa palestina na kusema kwamba "angalau nusu ya bidhaa zinazopita katika eneo la Kerem Shalom kwa sasa " zitaelekezwa katika eneo la Erez.

Israel inadhibitimaeneo yote yanayopakana na Ukanda wa Gaza, ispokua tu eneo la Rafah, linalodhibitiwa na Misri. Eneo la Erez lilifungwa mwaka 2008 kwa usafiri wa bidhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.