Pata taarifa kuu
PAKISTAN-TALIBAN-MAUAJI-MASHAMBULIZI

Hofu yatanda Pakistan baada watu 72 kuuawa

Wananchi wa Pakistan wameamka Jumatatu hii katika hali ya huzuni na masikitiko baada ya shambulizi la kujitoa mhanga lililotokea katika hifadhi ya manispa ya jiji la Lahore, Jumapili ya Pasaka, na kuua watu wasiopungua 72.

Watu 72, ikiwa ni pamoja na watoto 29, wameuawa Jumapili jioni 27 katika shambulio la kujitoa mhanga katika bustan la mjini Lahore, Pakistan.
Watu 72, ikiwa ni pamoja na watoto 29, wameuawa Jumapili jioni 27 katika shambulio la kujitoa mhanga katika bustan la mjini Lahore, Pakistan. ARIF ALI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watoto wengi ni miongoni mwa wahanga waliouawa katika shambulizi hilo na shambulio hili ni pigo kubwa kwa matumaini ya kuboresha usalama.

Shambulizi hili limedaiwa kutekelezwa na kundi la Taliban nchini Pakistan, ambalo limesema lilikua limeilenga jumuiya ya kikristo. Lakini kwa mujibu wa Naibu mkuu wa Polisi Haider Ashraf, wengi wa wahanga ni Waislamu.

Idadi ya waliouawa katika shambulio hilo imeongezeka mapema Jumatatu asubuhi na kufikia 72, naibu mkuu wa polisi amesema, akiliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP. Kwa mujibu wa afisa waIdara ya huduma za dharura, watoto 29 waliuawa pamoja na wanawake 7 na wanaume 36.

Mlipuko huo ulitokea katika Hifadhi ya Gulshan-e-Iqbal karibu na katikati mwa mji wenye wakazi milioni 10, ambapo kulikua na msongamano, hasa katika siku ya jana wakati Wakristo wamekua wakisherehekea Jumapili ya Pasaka.

Hayo yakijiri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelaani shambulizi hilo, akisem akwamba ni kitendo cha ujinga.

Moon ametaka maafisa wa serikali ya Pakistan kuwasaka na kuwachukua hatua wale wote waliohusika na shambulizi hilo la kigaidi.

Serikali ya Pakistan inasema itaendnelea kushirikiana na mataifa megine kama Saudi Arabia na Iran kuimarsiha usalama wake na kupambana na makundi ya kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.