Pata taarifa kuu
SYRIA-UPINZANI-MAZUNGUMZO

Syria: hatima ya Bashar al-Assad katika mazungumzo ya Geneva

Mazungumzo kati ya serikali ya Syria na Upinzani yenye lengo la kumaliza mgogoro nchini Syria yameanza Jumatatu hii katika mji wa Geneva chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa, lakini hatima ya Rais Bashar al-Assad inaweza kuzorotesha mchakato wa amani.

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura Machi 14, 2016 Geneva.
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura Machi 14, 2016 Geneva. PHILIPPE DESMAZES/AFP
Matangazo ya kibiashara

Msimamizi wa mazungumzo hayo, Staffan de Mistura, Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, amesema kuwa "suala mama" ni kufikiwa makubaliano kuhusu mabadiliko ya kisiasa. "Tupo katika wakati wa ukweli," ameongeza katika mkutano na waandishi wa habari katika utangulizi wa mkutano wake na kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Damascus, Bashar Bashar al-Jaafari.

Baada ya mkutano huo wa kwanza, ambao umedumu zaidi ya saa moja katika Jumba la Mataifa, Bw De Mistura ameeleza "aliruhusu "kufafanua masuala kadhaa, hususan masuala ya kiutaratibu." "Mkutano ujao (na serikali) Jumatano asubuhi utajikita kwenye ajenda, ambayo ni kama mnavyojua ile iliyowekwa na azimio 2254," De Mistura ameongeza.

Waraka huu, iliyopitishwa mwezi Desemba na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, unatoa uundwaji wa taasisi ya mpito nchini Syria ndani ya miezi 6 na uchaguzi ndani ya miezi 12.

Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa na mkuu wa ujumbe wa serikali ya Syria, Bashar al-Jaafari, Machi 14, 2016, Geneva.
Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa na mkuu wa ujumbe wa serikali ya Syria, Bashar al-Jaafari, Machi 14, 2016, Geneva. PHILIPPE DESMAZES/AFP

Kwa upande mwingine, Bw Jaafari amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba mkutano alikuwa "mzuri na wenye lengo la kujenga". Amesema alimpa Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa "mambo ya msingi kwa ufumbuzi wa kisiasa," lakini bila kutoa maelezo.

"Tunataka mazungumzo kati ya wadau wote nchini Syria, lakini bila masharti," ameongeza Bw Jaafari, balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa, akimaanisha madai ya upinzani ambao unadai kuondoka madarakani kwa Rais Assad, akiwa ameuawa au hai kabla ya ufumbuzi wowote wa kisiasa.

Assad na Putin wakubaliana juu ya uondoaji wa majeshi ya Urusi kutoka Syria

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Syria Bashar al-Assad walmekubaliana kwa njia ya simu juu ya uondoaji wa majeshi ya Urusi kutoka Syria, wakati huku wakisalia tu wanajeshi wa anga, Ikulu ya Urusi (Kremlin) imesema Jumatatu hii.

"Rais wa Urusi amesema kuwa operesheni kuu ziliombwa vikosi vya kijeshi zimekamilika. Suala lililoafikiwa ni uondoaji wa sehemu kubwa ya kikosi cha wanajeshi wa anga wa Urusi," Kremlin imesema katika taarifa yake, huku ikiongeza kuwa idadi ndogo ya wanajeshi wa anga itaendelea kuwepo kwa kuimarisha utekelezaji wa mkataba wa usitishwaji wa mapigano.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.