Pata taarifa kuu
SYRIA-MAZUNGUMZO

Upinzani Syria uko tayari kushiriki mazungumzo Geneva

Kamati Kuu ya Mazungumzo (HCN), ambayo inaleta pamoja makundi muhimu ya upinzani nchini Syria, imetangaza Ijumaa hii kwamba inajiandaa kushiriki mazungumzo ya Geneva kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo kwa mazungumzo na serikali.

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura Machi 3, 2016 Geneva.
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura Machi 3, 2016 Geneva. AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, HCN inasema kwamba watashiriki katika mazungumzo chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa, kwa kuzingatia "dhamira yake ya kushirikiana na juhudi za kimataifa za kukomesha umwagaji damu na kutafuta ufumbuzi wa kisiasa "kwa mgogoro wa Syria.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura ametangaza kuwa "majadiliano makubwa yataanza Machi 14 hadi Machi 24 au kabla ya terehe hiyo."

Ujumbe wa serikali ya Syria, ukiongozwa na balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa Bashar al-Jaafari, unasubiriwa Jumapili asubuhi, mwishoni mwa wiki hii mjini Geneva.

Katika taarifa yake, HCN imesema kwamba ingeliweza kuzungumzia "kuhusu kuundwa kwa serikali ya mpito yenye mamlaka zote za utawala" ambapo Rais Bashar al-Assad "hatopewa nafasi hata moja."

HCN inasema kwamba "haitoi masharti yoyote kwa kushiriki katika mazungumzo," lakini inasisitiza kuwa pande husika zinatakiwa kujiunga kwenye mikataba ya kimataifa juu ya masuala ya kibinadamu.

Mratibu Mkuu wa HCN Riad Hijab amesema kuwa ujumbe wake uko tayari "kutumia fursa zooteili kupunguza mateso yanayowakabili raia wa Syria."

Zaidi ya watu 270,000 wamepoteza maisha tangu kuanza kwa vita nchini Syria, Machi 15, 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.