Pata taarifa kuu
SYRIA-UN-MAZUNGUMZO

Syria: "serikali itashiriki mazungumzo Geneva"

Serikali ya Syria itashiriki katika mazungumzo ya amani yaliyopangwa machi 14,kwa mujibu wa utawala wa Damascus, upinzani bado haumua juu ya uwepo wake katika mazungumzo hayo yatakayofanyika mjini Geneva chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa.

Maandamano dhidi ya serikali ya Syria mjini Aleppo, Syria, Machi 7, 2016.
Maandamano dhidi ya serikali ya Syria mjini Aleppo, Syria, Machi 7, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Staffan de Mistura, alisema wiki iliyopita kwamba mazungumzo hayo yataanza Machi 10. Lakini chanzo cha karibu ya ujumbe wa serikali ya Syria kimesema kuwa "walipokea Jumapili usiku mwaliko wa Umoja wa Mataifa unaowtaka Machi 14 kushiriki maungumzo mjiniGeneva." "Bila shaka ujumbe wa serikali utashiriki kwa vile umealikwa," chanzo hicho kimelihakikisha shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Hata hivyo upinzani bado haujaamua iwapo utashiriki katika mazungumzo hayo au la.

Riad Naassan Agha, msemaji wa Ofisi ya kamati ya mazungumzo (HCN, ambayo inaleta pamoja makundi muhimu ya upinzani na waasi), amesema kuwa upinzani "umekubaliana kwenda Geneva" na ilikuwainatazamiwa kuwa "ujumbe wa upinzani utawasili Ijumaa" Machi 11.

Lakini masaa kadhaa baadaye, mratibu mkuu wa Ofisi ya kamati ya mazungumzo, Riad Hijab, alitangaza kuwa HCN "itatathmini hali katika siku zijazo na kuchukua uamuzi sahihi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.