Pata taarifa kuu
GHUBA-HEZBOLLAH-UGAIDI

Nchi za Ghuba zatangaza Hezbollah kuwa ni magaidi

Kundi la Kishia kutoka nchini Lebanon la Hezbollah limetangazwa Jumatano hii kuwa ni "kundi la kigaidi". Uamzi huo umechukuliwa na tawala sita za nchi za Ghuba.

Waislamu wa Kishia wakibebelea mabango yenye picha za kiongozi wa Hezbollah, Sayyed Hassan Nasrallah (kushoto) na Rais wa Syria Bashar Assad wakati wa mkutano wa hadhara dhidi ya kuingilia kwa mataifa ya kigeni nchini Syria, mjini Sanaa, Agosti 30, 2013.
Waislamu wa Kishia wakibebelea mabango yenye picha za kiongozi wa Hezbollah, Sayyed Hassan Nasrallah (kushoto) na Rais wa Syria Bashar Assad wakati wa mkutano wa hadhara dhidi ya kuingilia kwa mataifa ya kigeni nchini Syria, mjini Sanaa, Agosti 30, 2013. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Saudi Arabia, Bahrain, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Oman na Kuwait wanalishtumu kundi la Hezbollah "kutekeleza na kuchochea vitendo vya kigaidi nchini Syria, Yemen na Iraq."

Hii ni sehemu mpya ya mapambano kati ya tawala za nchi za Ghuba (ikiongozwa na na Saudi Arabia) kwa upande mmoja na kwa upande mwingine, Iran na washirika wake wa kikanda. Pamoja na hayo Hezbollah, ambayo ni chama cha siasa kundi la wapiganaji kutoka jamii Mashia nchini Lebanon.

Hezbollah inaendesha harakati zake nchini Syria, ambako inasaidia kijeshi utawala wa Bashar al-Assad. Tawala za nchi za Ghuba - Waarabu kutoka jamii ya Masuni - wanaishtumu Hezbollah kuwa inachangia katika kuibuka kwa migogoro mingine ya kikanda na hasa nchini Yemen, pamoja na kulisaidia kundi la waasi la Kishia dhidi ya muungano wa kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia ulioingilia kijeshi nchini Yemen kwa karibu mwaka mmoja sasa.

Athari nchini Lebanon

Siku hizi, vita vya maeneo au makabiliano ya kikanda kati ya tawala za nchi za Ghuba na Iran yameleta athari kubwa nchini Lebanon. Saudi Arabia iliomba hivi karibuni raia wake kuondoka Lebanon. Iliwataka raia wake kufuta safari katika nchi hii ya Lebanon. Pia ilisimamisha mpango wa kulisaidia jeshi la Lebanon. Mpango huo umekua ukigharimu Dola bilioni 3 kwa mwaka. Vie vile iliyawekea vikwazo makampuni na wafanyabiashara wanaochukuliwa kuwa ni washirika wa karibu wa Hezbollah.

Hali hii inatokea wakati ambapo Lebanon inaendelea kukabiliwa na hali ngumu ya kiusalama na siasa. Nchi hii inakabiliwa na hali ya sintofahamu kwa karibu miaka miwili kutokana na mgogoro mkubwa wa kisiasa, kwa upande mmoja, Hezbollah na washirika wake na, kwa upande mwingine, kambi ya kisiasa inayoungwa mkono na Saudi Arabia.

Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah alisema Jumanne Machi 1 kwamba Saudi Arabia haipaswi kuwaadhibu raia wa Lebanon kwa sababu pekee ya kuwa na tofauti za kisiasa na Lebanon pamoja na Hezbollah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.