Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-ONYO-MASHAMBULIZI

Israel: mkuu wa majeshi hataki matumizi ya nguvu

Hili ni onyo ambalo halikutarajiwa kwa kulenga matumizi ya nguvu ya vikosi vya usalama na ulinzi dhidi ya Wapalestina. Onyo hili limetolewa na mkuu wa majeshi ya Israel mwenyewe.

Gadi Eizenkot, namba moja wa majeshi la Israel, picha ya Februari 16, 2016, Tel Tel Aviv.
Gadi Eizenkot, namba moja wa majeshi la Israel, picha ya Februari 16, 2016, Tel Tel Aviv. AFP PHOTO / JACK GUEZ
Matangazo ya kibiashara

Gadi Eizenkot alikumbusha Jumatano hii Februari 17 kwamba wanajeshi wake wanapaswa kufuata baafhi ya sheria, wakati ambapo wimbi la ghasia limeendelea kuukabili mji wa Jerusalem, nchi nzima ya Israel na maeneo ya Palestina kwa zaidi ya miezi minne. Tangu wakati huo, Wapalestina 172 waliuawa. Wengi walihumiwa kutekeleza au la baada kutaka kutekeleza mashambulizi kwa visu. Waisrael ishirini na sita waliuawa.

Hotuba hiyo imerushwa hewani kwenye runinga ya Israel. mkuu wa majeshi ya Israel Gadi Eizenkot alikua akizungumza katika shule moja ya sekondari wakati alieleza kuhusu jinsi askari wanapaswa kukabiliana na mashambulizi ya Wapalestina : "Wakati msichana mwenye umri wa miaka 13 anashikilia mkasi au kisu, ili hali kuna umbali kati yake na askari, sitaki kuona askari anafungua moto na kumuua bila sababu zozote zile, hata kama atakua ametenda kitendo kibaya sana. "

Wito huu wa kujizuia kutoka kwa mkuu wa majeshi unakinzana na kauli ya serikali ya Israel. Serikali ya Israel imekua ikitolea wito wa kukabiliana vilivyo dhidi ya mashambulizi, huku ikivipa idhini vikosi vya usalamakutekeleza kazi yao ipasavyo. Mashambulizi haya ya kupambana na Israel yanaendeshwa mara nyingi na vijana wa Palestina wenye umri mdogo wakibebelea visu.

Wito kutoka mataifa mbalimbali umekua ukitolewa kwamba inawezekana katika baadhi ya kesi, kuwakamata vijana hao bila kuwaua. Mashirika ya haki za binadamu ya Israel, lakini pia viongozi mbalimbali wa kigeni, kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, walionya dhidi ya matumizi ya nguvu ya vikosi vya usalama na ulinzi vya Israel. Viongozi hao walituhumiwa na serikali ya Israel kwamba "wanaunga mkono ugaidi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.