Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI-URUSI-VITA

Syria: vita vya maneno kati ya Ankara na Moscow

Vikosi vya Kikurdi nchini Syria vimekua vikisonga mbele Jumatatu hii kaskazini mwa Syria licha ya mashambulizi ya Uturuki, huku vita vya maeneo vikiendelea kushuhudiwa kati ya Ankara na Moscow.

Jengo la hospitaliinayosaidiwa na Madaktari wasio na Mipaka (MSF) Februari 15, 2016 katika mji wa Maaret al-Noomane, Syria.
Jengo la hospitaliinayosaidiwa na Madaktari wasio na Mipaka (MSF) Februari 15, 2016 katika mji wa Maaret al-Noomane, Syria. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kaskazini magharibi mwa Syria, hospitali inayosaidiwa na Madaktari wasio na Mipaka (MSF) imelengwa na mashambulizi ya anga ya Urusi, na kuua watu wasiopungua saba na wafanyakazi wanane wametoweka, kwa mujibu wa shirika hilo lilsilokua la kiserikali.

Matumaini ya makubaliano ya usitishwaji mapigano yameonekana kutofanikiwa Jumatatu hii nchini Syria, ambako watu hamsini wakiwemo watoto wameuawa na makombora yaliyorushwa katika hospitali na shule, Umoja wa Mataifa umelaani "ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa."

Vita vya maneno kati ya Moscow na Ankara vimeendelea kushuhudiwa, hivyo kuonyesha jinsi gani mgogoro wa Syria umeingiliwa kimataifa. Urusi, mshirika mkuu wa utawala wa Bashar al-Assad imeshutumu "vitendo vya uchokozi" vinavyoendeshwa na Uturuki. Urusi imesema Uturuki imeendelea "kuunga mkono kiuficho ugaidi wa kimataifa".

Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amejibu akishutumu Urusi kwa kuwa na tabia "kama kundi la kigaidi" nchini Syria ambapo inaongoza, kama wanajihadi wa kundi la Islamic State (IS) "mashambulizi ya kikatili dhidi ya raia". "Kama wataendelea", "tutakabiliana nao", Waziri Mkuu wa Uturuki ameonya.

Vita hivi vya maneno vinafuatiwa na kuongezeka kwa wasiwasi kwa nchi za magharibi, ambazo zinaonekana kutokua na uwezo wa kukomesha hali hii

Vita hivi vya maeneo vinatokea wakati ambapo jeshi la Uturuki limeendelea kwa siku ya tatu mfululizo, kushambulia ngome za wapiganaji wa Kikurdi karibu na mpaka wa Syria na Uturuki katika jimbo la kaskazini la Aleppo.

Jumatatu hii, balozi wa Syria mjini Moscow, Riad Haddad, ameituhumu Marekani kutumia ndege yake kwa kuendesha mashambulizi katika hospitali inayosaidiwa na shirika la Madaktari wasio na Mipaka (MSF) katika mkoa wa Idleb, akitupilia mbali shutuma za Washington zinazoihusisha serikali ya Syria na mshirika wake Urusi katika mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.