Pata taarifa kuu
IS-JIHAD JOHN

IS yathibitisha kifo cha muaji mkuu"Jihadi John"

Katika taarifa iliyorushwa hewani na kuchapishwa kwenye mtandao, kundi la Islamic State imethibitisha kifo cha raia wa Uingereza "Jihadi John", ambaye aliuawa mwezi Novemba mwaka jana katika mashambulizi dhidi ya ngome yake kuu mjini Raqqa nchini Syria.

kundi la IS limethibitisha kifo cha Jihadi John akijulikana kwa jina halisi Mohammed Emwazi
kundi la IS limethibitisha kifo cha Jihadi John akijulikana kwa jina halisi Mohammed Emwazi Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Jihadi John", ambaye jina lake halisi ni Mohammed Emwazi, alionekana katika video kadhaa za IS, ambapo alionekana akijificha uso na kuwaua mateka kutoka nchi za Magharibi. Alikua mtu muhimu katika kundi hili la Islamic State.

Katika gazeti lake, kundi la Islamic State limetoa rambirambi zake kwa mpiganaji wake Jihadi John, likithibitisha kifo chake kwa mara ya kwanza. Muuaji huyo maarufu wa kundi la IS ameelezwa katika jarida la propaganda la kundi hili la kigaidi la Dabiq kama mtu wa huruma na mwenye wema mkubwa.

Ishara ya wema, kundi la IS limeandika, siku moja aliletewa mtumwa mwanamke hakusita kumfanya zawadi kwa mpiganaji mwingine aliekuwa amejeruhiwa na ambaye alikua hajaoa. Hata hivyo hakuna kumbukumbu ya mauaji ya mateka kutoka nchi za Magharibi akitumia kisu, kama ilivyoonekana katika video ya waandishi wa habari wa Marekani James Foley na Steven Sotloff ambayo ilimfanya maarufu, akijificha uso, huku akivalia nguo nyeusi akimtishia Barack Obama katika lugha ya Kiingereza.

Hakuna kumbukumbu pia alipokuwa mwanamuziki wa mtindo wa Rap, wakati alipokua akiishi mjini London, nchini Uingereza. Akiwa na umri wa miaka ishirini, Abu Mouharib al-Muhadjir jina lake pia, Mohammed Emwazi jina lake halisi, alizaliwa nchini Kuwait, mama yake ni raia wa Yemen, kwa mujibu wa kundi IS, ikithibitisha taarifa iliotangazwa na Marekani. Mwezi Novemba mwaka jana, mtu huyo ambaye mateka walimpa jina la utani la "Jihadi John" aliuawa katika shambulio la ndege isio narubani dhidi ya gari lake katika mji wa Raqqa, nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.