Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-SHAMBULIZI

Afghanistan: raia 1 auawa katika shambulizi la kujitoa mhanga Kabul

Shambulio la kujitoa mhanga kwa gari linalodaiwa kutekelezwa na kundi la Taliban, limemuua mtu mmoja Jumatatu hii katika mji wa Kabul, siku moja baada ya kutangazwa kwa mpango wa kufufua mchakato wa amani na wapiganaji.

Shambulio la kujitoa mhanga Desemba 28, 2015 katika mji wa Kabul.
Shambulio la kujitoa mhanga Desemba 28, 2015 katika mji wa Kabul. AFP
Matangazo ya kibiashara

Inasemekana kuwa shambulizi hilo limekua limelenga msafara wa magari ya kijeshi ya NATO.

Shambulizi hilo, limetokea karibu na uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Afghanistan, "limemua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine 13", Abdul Basir Mujahid, msemaji wa polisi katika mji wa Kabul, amesema. Shambulizi hilo limekua limelenga "msafara wa magari ya magari ya askari wa kigeni", Najib Denmark, kutoka Wizara ya mambo ya ndani amesema.

Wapiganaji wa Taliban mara nyingi hulenga misafara ya magari ya askari wa kigeni waliotumwa nchi humo, ambapo inawachukulia kama "wavamizi".

Wapiganaji, kupitia msemaji wao wa kawaida Zabiullah Mujahid, wamekiri maramoja kwenye Twitter kwamba wamehusika na shambulizi hilo, na kuthibitisha kwamba askari "wengi" wa kigeni wameuawa. Kundi la Taliban mara nyingi linaongeza idadi watu au kiwango cha hasara ya mashambulizi yake dhidi ya Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO.

Askari sita wa Marekani wa Ujumbe wa NATO waliuawa wiki moja iliyopita katika shambulio la kujitoa mhanga lililodaiwa kutekelezwa na wapiganaji Taliba karibu na kambi ya jeshi la Marekani ya Bagram, kaskazini mwa mji wa Kabul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.