Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Pakistan: watu 23 wauawa katika shambulio la Wasuni wenye msimamo mkali

media Hospitali kuu ya Parachinar(kaskazini magharibi mwa Pakistan) ambapo watu waliojeruhiwa baada ya mashambulizi ya bomu wamekua wakiletwa, Desemba 13, 2015. AFP/AFP

Watu wasiopungua 23 wameuawa na zaidi ya 30 wamejeruhiwa Jumapili hii na mlipuko wa bomu katika eneo la kaskazini magharibi mwa Pakistan, shambulizi ambalo limeidaiwa jioni kutekelezwa na kundi la Wasuni wenye msimamo mkali la Lashkar-e Jhangvi.

"Tunawaonya wazazi wa Kishia, kama hawawazuia watoto wao kushiriki katika vita vya Bashar Al Assad, kutakuwa na mashambulizi zaidi kama haya", amesema Ali Bin Sufiyan, ambaye anachukuliwa kama msemaji wa kundi la Lashkar-e-Jhangvi, katika ujumbe uliotumwa kwa vyombo vya habari.

Kundi hili lenye mafungamano na Al-Qaeda, linawatuhumu Mashia kumuunga mkono rais wa Syria Bashar Al Assad na Iran. Kiongozi wa kundi hili, Malik Ishaq, mwenye umri wa miaka 55, aliuawa Julai mwaka jana pamoja na washirika wake 13 wa karibu katika operesheni ya polisi.

Bomu, lililokuwa limefichwa katika mfuko, limepuka katika soko la mavazi la Eidgah Parachinar, mji wenye wakazi wengi kutoka jamii ya watu wachache ya Mashia na unapatikana katika eneo lenye mzozo wa kikabila la Kurram, kwa mujibu wa maafisa wa serikali.

"Idadi ya waliouawa imefikia 23 kwani baadhi ya watu waliojeruhiwa vibaya wamefariki wakati walipokua wakisafirishwa kwa helikopta katika mji wa Peshawar", Amjad Ali Khan, mkuu wa wilaya ya Kurram, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Maafisa wawili wa utawala katika eneo hilo wamethibitisha vifo hivyo. Jeshi limethibitisha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba helikopta mbili za jeshi zimetumwa eneo hilo ili kusafirisha watu waliojeruhiwa.

Runinga za eneo hilo zimerusha hewani picha zinazoonyesha mamia ya watu waliokimbia eneo kulikotokea shambulio hilo, huku magari ya wagonjwa yakisafirisha miili ya watu waliouawa na watu waliojeruhiwa.

Eneo hili la mizozo ya kikabila la kaskazini magharibi mwa Pakistan limekua likilengwa na mashambulizi ya kundi la Taliban, kutoka Afghanistan na Pakistan, na makundi mengine yenye uhusiano na Al Qaeda.

Mji wa Parachinar, ulio karibu na mpaka wa Afghanistan, ulishuhudia mashambulizi yaliosababisha vifo vya watu wengi katika miaka ya hivi karibuni, kwa sababu unakaliwa na wakazi wengi kutoa jamii ya Mashia.

Mashia, wamekua wakilengwa na mashambulizi ya makundi mengi yenye msimamo mkali yakiwashtumu kuharibu Uislamu na kuwa maafisa wa ujasusi wa Iran, nchi yenye nguvu yenye Mashia wengi duniani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana