Pata taarifa kuu
LEBANON-MAUAJI-USALAMA

Watu 37 wameuawa katika mashambulizi Beirut

Kwa uchache watu 37 wameuawa na 181 kujeruhiwa Alhamisi hii katika mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga yaliotokea katika ngome kuu ya Hezbollah katika kitongoji kimoja cha mji wa Beirut, Shirika la Msalaba Mwekundu la Lebanon na polisi vimebaini.

Maafisa wa Idara ya huduma za dharura katika eneo mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga katika mji wa Beirut Novemba 12, 2015.
Maafisa wa Idara ya huduma za dharura katika eneo mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga katika mji wa Beirut Novemba 12, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Idadi ya wato waliouawa bado imesimamia kwenye 37 na angalau 181 waliojeruhiwa", Shirika la Msalaba Mwekundu limeliambia Shirika la habari la Ufaransa la AFP. Kwa mujibu wa polisi, watu wawili walokua wakitembea kwa miguu wamelipua mikanda yao iliokua imejaa vilipuzi mbele ya kituo cha biashara cha mtaa wa al-HussiniyΓ© cha eneo la Bourj al-BarajnΓ©.

Mashambulizi haya mawili yametokea saa 12:00 jioni saa za Lebanon )sawa na saa 10:00 Alaasiri saa za kimataifaya).

Mpiga picha wa shirika la habari la Ufaransa la AFP aliona miili iliyojaa damu katika maduka na madonge ya damu katikati ya magari, wakati ambapo mamia ya watu walikuwa maeneo jirani.

"Tuna majeruhi kadhaa na wanaendelea kuwasili", daktari wa Hospitali ya Bahman katika wilaya jirani ya Haret Hreik ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Hili ni shambulizi la kwanza dhidi ya ngome ya kundi la Kishia la Hezbollah tangu Juni 2014. Afisa wa usalama aliuawa wakati huo akizuia shambulio la gari lililokua lilitegwa bomu. Awali mashambulizi kadhaa mengine yalisababisha vifo vya watu katika ngome ya Hezbollah nchini Lebanon kati ya Julai 2013 na Februari 2014, mashambulizi yalidaiwa kutekelezwa na makundi yenye msimamo mkali ya Wasuni.

Wakati huo huo kundi la Islamic State limekiri kuhusika namashambulizi hayo mawili katika mji wa Beirut.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.