Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-MAREKANI-SAUDIA-USALAMA

Mkutano mjini Vienna juu ya Syria: hatma ya Assad yasababisha mgawanyiko

Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani, Urusi, Uturuki na Saudi Arabia wamekutana Alhamisi Oktoba 29 mjini Vienna ili kutafutia ufumbuzi wa kisiasa mgogoro wa Syria. Mazungumzo hayo yanatazamiwa kuendelea leo Ijumaa.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Urusi, Marekani na Saudi Arabia wakikutana katika mji wa Vienna, Oktoba 29, 2015, siku moja kbala ya mkutano wa kimataifa juu ya Syria.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Urusi, Marekani na Saudi Arabia wakikutana katika mji wa Vienna, Oktoba 29, 2015, siku moja kbala ya mkutano wa kimataifa juu ya Syria. AFP PHOTO / POOL / BRENDAN SMIALOWSKI
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo, ambao ulitanguliwa na mazungumzo kati ya Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Iran Javad Zarif, utafuatiwa leo Ijumaa katika mji mkuu wa Austria na mkutano wazi kabisa.

Nafasi ya Bashar Assad katika mchakato wa mpito wa kisiasa wa baadaye itagubika mazungunzo hayo.

Kwa mujibu wa John Kerry, mazungumzo katika mji wa Vienna ni nafasi nzuri ya "kutoka katika moto ". Kwa mara ya kwanza, wadau wote kutoka nje katika vita vya wenyewe kwa nchini Syria wako katika meza ya mazungumzo. Tehran, ambayo inamuunga mkono Assad, haikushiriki katika mazungumzo ya kwanza na ya pili mjini Geneva mwaka 2012 na 2014.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani mekutana Alhamisi hii mchana na mwenzake wa Iran Mohammad Javad Zarif, kabla ya kukutana na wawakilishi wa Urusi, Uturuki na Saudi Arabia kwa mkutano wa kwanza. Leo Ijumaa, wajumbe wengine kutoka Iran na Ufaransa, watajiunga katika mazungumzo hayo. Mazungumzo hayo yatagubikwa na suala la nafasi ya Bashar Al Assad katika mchakato wa mpito wa kisiasa wa baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.