Pata taarifa kuu
SYRIA=URUSI-MAREKANI-USALAMA

Syria: mazungumzo mjini Vienna kati ya Moscow na Washington na Ankara-Riyadh

Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani, Saudi Arabia, Uturuki na Urusi wanakutana leo Ijumaa katika mji mkuu wa Austria, Vienna, kwa ajili ya mazungumzo yasiyokuwa ya kawaida kuhusu vita vinavyoendelea nchini Syria kati ya Washington, Riyadh na Ankara, wapinzani wakali wa utawala wa Bashar Al Assad, na Moscow, mshirika wake mwaminifu.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov na Marekani John Kerry, Septemba 30, 2015 mjini New York
Mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov na Marekani John Kerry, Septemba 30, 2015 mjini New York Dominick Reuter/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Mji mkuu wa Austria utashuhudia tukio lisilokuwa la kawaidia kwa kuwapokea mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, Wa Urusi Serguei Lavrov, wa Saudi Arabia Al-Adel Jubeir na wa Uturuki Feridun Sinirlioglu.

Nchi nne zitashiriki mkutano huo ambao unatazamiwa kuanza kwa kina mapema mchana leo Ijumaa. Mkutano ambao utahusu mgogoro wa Syria, mjadala wa kwanza wa kidiplomasia na ishara ya kunyoshesha jinsi gani vita hivyo vinayashirikisha mataifa mengi. Vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria vimewauwa zaidi ya watu 250,000 tangu Machi 2011.

Mkutano usiyokuwa wa kawaida kati ya nchi tatu ikiwa ni pamoja na Marekani, Saudi Arabia na Uturuki, pia umepangwa kufanyika leo Ijumaa asubuhi. Mkutano huo utauatiwa mazungumzo kati ya John Kerry na Lavrov, viongozi wawili ambao wanaonyesha ushirikiano fulani na ambao wanadhibiti njia ya mawasiliano kati ya serikali zao kwa mahusiano duni.

Misimamo kati ya Washington, Riyadh na Ankara kwa upande mmoja na Moscow, kwa upande mwengineimeendelea kutofautiana kuhusu Syria.

Marekani na washirika wake wanadhibiti muungano wa kijeshi wa kimataifa dhidi ya kundi la Islamic State (IS) na kutoa msaada kwa waasi wa Syria, ambao wanachukuliwa kuwa maadui wa serikali ya Damascus.

Urusi, ambaye ni mshirika muhimu wa Rais Bashar al-Assad, imeanzisha mashambulizi ya anga wiki tatu zilizopita nchini Syria. Operesheni dhidi ya "ugaidi," Moscow imesema. Mashambulizi ambayo yanalenga kumsaidia Rais wa Syria, washington na washirika wake wametuhumu.

Kabla ya kumtumaWaziri wake Lavrov mjini Vienna, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitaja Alhamisi wiki hii kuwa " Lengo la Marekani ilikuwa kumuondoa madarakani Assad."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.