Pata taarifa kuu
URUSI-SYRIA-USHIRIKIANO-USALAMA

Bashar Al-Assad akutana na Vladimir Putin Moscow

Rais wa Syria Bashar Al Assad, amefanya ziara ya kikazi mjini Moscow Jumanne jioni wiki hii, ambapo alikutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, msemaji wa Kremlin, Dmitri Peskov, ametangaza.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Syria Bashar Al-Assad, Oktoba 21, 2015 Moscow.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Syria Bashar Al-Assad, Oktoba 21, 2015 Moscow. AFP/RIA NOVOSTI/AFP
Matangazo ya kibiashara

" Jumanne jioni, Rais wa jamhuri ya Kiarabu ya Syria, Bashar Al Assad, alikuja katika ziara ya kikazi mjini Moscow”, amesema Dmitri Peskov, ambaye alinukuliwa na mashrika ya habari ya Urusi, yakiongeza kuwa Bashar Al Assad amekutana kwa mazungumzo na Vladimiri Putin laikini bila kueleza kama Rais wa Syria bado yuko Moscow.

Hii ni ziara ya kwanza ya Bashar Al Assad ugenini tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011.

Urusi imekua ikilaumiwa kutokana na msaada wa kijeshi inayotoa kwa Bashar Al Assad, hasa ushirikiano wa majeshi ya Urusi na yale ya Syria yanayouunga mkono utawala wa Bashar Al Assad katika vita dhidi ya kile wanachokiita ugaidi.

Hayo yakijiri, Urusi na Marekani zimetia saini mkataba wa kuhakikisha kuwa ndege zao za kivita hazishambuliani nchini Syria.

Urusi na Marekani zinashiriki katika Operesheni ya kuwakomeza wapiganaji wa Islamic State.

Juma lililopita, ndege za nchi hizo mbili zilivamia eneo moja na kuzua hali ya wasiwasi na uwezekano wa kushambuliana.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje, Peter Cook, amesema Urusi imeomba kuwepo kwa mkataba huo ili kuzuia mgongano wowote katika Operesheni hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.