Pata taarifa kuu
SYRIA=URUSI-MAREKANI-USALAMA

Syria: mashambulizi ya jeshi Damascus yazua kizaaza

Vikosi vya serikali ya Syria vimeanzisha oparesheni kabambe ili kuwatimua waasi wanaokaribia mji wa Damascus, wakati ambapo Urusi na Marekani wanatazamiwa kuanzisha upya mazungumzo ili kuepuka tukio lolote kati ya ndege zao zinazoendesha mashambulizi ya anga nchini Syria.

Picha iliyotolewa na jeshi la Syria kuonyesha magari ya kijeshi ya Syria yanayopelekwa magharibi mwa nchi hiyo, Oktoba 8, 2015.
Picha iliyotolewa na jeshi la Syria kuonyesha magari ya kijeshi ya Syria yanayopelekwa magharibi mwa nchi hiyo, Oktoba 8, 2015. AFP/SANA/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Mapigano yamekua yakiendelea pia kaskazini mwa Aleppo, mji wa pili wa Syria, ambapowapiganaji wa kundi la Islamic State (IS) wamefunga barabara muhimu kwa waasi.

Katika vita ngumu inayoziahusisha nchi nyingi, Uturuki pia imeonya mataifa haya mawili yenye nguvu, Urusi na Marekani dhidi ya msaada wowote kwa kwa Wakurdi, maadui wakubwa wa serikali ya Ankara, Urusi na Marekani wanapambana dhidi ya kundi la Islamic State kaskazini mwa Syria.

Chanzo cha kijeshi nchini Syria kimeliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kwamba vikosi vya serikali vimesonga mbele Jumatano katika mji wa Jobar, mashariki mwa Damascus ili kujaribo kuwatimua wapiganaji ambao wameizungula sehemu kubwa ya mji mkuu wa nchi hiyo.

"Jeshi limeanza operesheni ya kijeshi Jumatano hii asubuhi kwa lengo la kupanua eneo la usalama kando na maeneo yanayodhibitiwa na jeshi ", chanzo hicho kimesema. Ndege za jeshi la Syria zinaendelea na mashambulizi lakini siondege za Urusi , kwa mujibu wa chanzo hicho.

Mshirika wa karibu wa Rais Bashar Al-Assad, Urusi ilianza mashambulizi ya anga Septemba 30dhidi ya makundi ya " kigaidi " nchini Syria, ikimaanisha kwa wale wanaopinga utawala wa Bashar Al Assad.

Balozi wa Urusi nchini Syria amesema Jumatano wiki hii kwamba idadi ya wapiganaji waliyowasilishwa na nchi za Magharibi kama " waasi " walikuwa tu " wenye msimamo mkali " na " magaidi ".

Urusi tangu wakati huo ilianza kulengwa na kundi la Islamic State, ambalo lilitolea wito Jumanne wiki hii kuanzisha vita vitakatifu dhidi yake kama dhidi ya Marekani. " Urusi itashindwa ", ameonya msemaji wa kundi hilo, Abu Mohamed al-Adnani, katika mkanda uliyorekodiwa kwenye mtandao wa wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.