Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-MAREKANI-MAPIGANO-USALAMA

Jeshi la Syria lasonga mbele, Washington yawapa silaha waasi

Jumatatu wiki hii jeshi la Syria likisaidiwa na ndege za Urusi limesonga mbele katika uwanja wa mapigano katika maeneo mbalimbali yanayokaliwa na waasi.

Picha iliyochukuliwa kutoka video iliyorushwa hewani Oktoba 12, 2015 kwenye tovuti ya wizara ya ulinzi ya Urusi ikionyesha mashambulizi ya anga ya Urusi katika kambi ya mafunzo ya kundi la Islamic State.
Picha iliyochukuliwa kutoka video iliyorushwa hewani Oktoba 12, 2015 kwenye tovuti ya wizara ya ulinzi ya Urusi ikionyesha mashambulizi ya anga ya Urusi katika kambi ya mafunzo ya kundi la Islamic State. AFP/Ministère russe de la Défense/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wake Umoja wa Ulaya umeshutumu msaada wa Moscow kwa utawala wa Bashar al-Assad.

Marekani, ambayo pia inapinga Urusi kuingilia kijeshi katika vita nchini Syria, imeamua kusaidia waasi wengine wanaopigana dhidi ya wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS), ambapo Jumapili mwishoni mwa juma lililopita iliwadondoshea silaha na vifaa vingine vya jeshi, kaskazini mwa Syria.

Katika mgogoro huu mgumu kufuatia nchi nyingi kuingilia katika vita vinavyoendelea nchini Syria, Urusi imeendelea kumsaidia Bashar Al Assad ikibaini kwamba wale wote wanaompinga rais huyo kwa njia ya mtuto ni kama "magaidi", wakati ambapo Marekani na Umoja wa Ulaya wanaosisitiza juu ya kuondoka kwa Bashar Al Assad, wanayasaidia makundi ya waasi wanaoyachukulia kuwa ni yenye msimamo wa "wastani" na wanataka hasa kulitokomeza kundi la Islamic State (IS).

Akisisitiza juu ya mchakato wa kisiasa ili kumaliza mgogoro unaoendelea, mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Syria Staffan de Mistura anatazamia kusafiri Jumatatu katika miji ya Moscow na Washington. " Ni wazi kwamba Urusi kuingilia kijeshi nchini Syria kumepelekea kuanzishwa nguvu mpya ", amesema Staffan de Mistura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.