Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-NATO-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan: askari wa NATO washirikiana na jeshi la Afghanistan

Vikosi maalum vya Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO vimetumwa katika jimbo la Kunduz kusaidia wenzao wa Afghanistan kuweka kwenye himaya yao mji huo muhimu wa Kaskazini mwa Afghanistan, uliyoanguka mikononi mwa waasi wa Taliban, msemaji wa vikosi vya Marekani kanali Brian Tribus ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Vikosi vya usalam vya Afghanistan karibu na uwanja wa ndege wa Kunduz, Septemba 29, 2015.
Vikosi vya usalam vya Afghanistan karibu na uwanja wa ndege wa Kunduz, Septemba 29, 2015. NASIR WAQIF/AFP
Matangazo ya kibiashara

Chanzo cha kijeshi cha Magharibi, ambacho hakikutaka kutajwa, kwa upande wake, kimesema wanajeshi wazowefu kutoka Marekani, Uingereza na Ujerumani, ni sehemu ya askari 13,000 wa kigeni ambao bado wanasalia nchini Afghanistan.

Tangu kuondoka kwa vikosi vingi vya Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi (NATO) Desemba mwaka jana, askari wa kigeni wanaosalia nchini Afghanistan wamebaki tu na jukumu la kutoa ushauri na mafunzo ya majeshi ya Afghanistan.

Akihojiwa na AFP, kanali Tribus amekataa kueleza idadi ya askari waliotumwa na maudhui ya kazi yao (ushauri / mafunzo au mapambano) katika jimbo la Kunduz.
Kanali Brian Tribus ameongeza kuwa jeshi la Marekani limeendesha usiku Jumanne kuamkia Jumatano mashambulizi ya anga mapya mawili. Shambulio la kwanza limetekelezwa saa 5:30 na la pili saa 7:00 Jumatano, " karibu na uwanja wa ndege " wa Kunduz. Hakueleza maeneo yaliyolengwa.

Mpigano makali katika ya Taliban na jeshi yametokea usiku katika uwanja wa ndege, kilomita 10 kutoka katikati ya mji, ambapo wapiganaji wameweza kusonga mbele hadi eneo hilo, licha ya Rais Ashraf Ghani kuhakikisha kuwa " vikosi vya serikali vinaelekea katika mji wa Kunduz. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.