Pata taarifa kuu
AFSTAN-MAPIGANO-USALAMA

Afghanistan: kundi la Taliban ladhibiti nusu ya Kunduz

Kwa mara ya kwanza tangu kuanguka kwa utawala wao mwaka 2001, waasi wa Taliban wameingia katika mji mkubwa wa Afghanistan, Kunduz, mji muhimu wa kaskazini mwa nchi ya Afghanistan, na kusababisha pigo kubwa kwa serikali ya Afghanistan iliyoundwa mwaka mmoja uliyopita.

Vikosi vya usalama vya Afghanistan vikikusanyika katika mji wa Kunduz nchini Afghanistan, Septemba 28, 2015.
Vikosi vya usalama vya Afghanistan vikikusanyika katika mji wa Kunduz nchini Afghanistan, Septemba 28, 2015. Gul RAHIM | AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi kadhaa, wakazi wamejikuta Jumatatu wiki hii wakizungukwa na waasi katika mji huo mkubwa wa kibiashara wenye wakazi 300,000. Kunduz ni mji unaounganisha barabara inayoelekea Kabul na Tajikistan.

" Baada ya kuanzisha mashambulizi yao mapema Jumatatu alfajiri wiki hii, wapiganaji wameingia katika mji huo Jumatatu mchana, na saa chache baadaye walikua tayari kudhibiti nusu ya mkoa huo ", Sayed Sarwar Hussaini, msemaji wa polisi wa mkoa wa Kunduz amesema.

" Majeshi yanayokuja kutusaidia bado hayajafikia askari wetu. Mapigano yanaendelea", Sayed Sarwar Hussaini ameiambia televisheni ya Afghanistan.

Wapiganaji wa Taliban pia wamepandisha bendera yao nyeupe kwenye eneo kuula mji wa Kunduz, kwa mujibu wa kiongozi wa eneo hilo ambaye amezungumza kwa masharti ya kutotajwa, taarifa ambayo haikuthibitishwa rasmi.

Na, kama katika kitendo cha dharau, wapiganaji wa Taliban wanakisiwa kuwa wamewaachilia huru mamia ya wafungwa, ikiwa ni pamoja na wapiganaji wa Taliban, kutoka katika gereza la mji, kwa mujibu wa chanzo hicho.

Katika mji wa Kunduz, wakazi wamesalia mafichoni nyumbani, kwa mujibu wa msaidizi wa shirika a habari la Ufaransa la AFP. " wapiganaji wa Taliban wamechukua udhibiti wa kata yetu, naona wapiganaji wao ", amesema kiongozi huyo.

" Nyumba yangu inapatikana mita 100 kutoka eneo ambapo wapiganaji wa Taliban wamepiga kambi ", amesema afisa huyo wa kikabila. " Wapiganaji wamepandisha bendera yao nyeupe kwenye eneo la maduka ", Javed, fundi cherehani katika mji wa Kunduz ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.