Pata taarifa kuu
MALAYSIA-SIASA

Waziri mkuu wa Malaysia aombwa kujiuzulu

Shinikizo zaidi la kujiuzulu kwa Waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak limeendelea kueongezeka, huku waandamanaji wakipewa nguvu zaidi na aliyewahi kuwa kiongozi wa muda mrefu nchini humo, Mahathiri Mohamad ambaye aliungana na waandamanaji.

Raia wa malaysia waandamana wakimtaka waziri mkuu wa Najib Razak kujiuzulu, wakimtuhumu kujihusisha na kashfa za rushwa, Agosti 29, 2015.
Raia wa malaysia waandamana wakimtaka waziri mkuu wa Najib Razak kujiuzulu, wakimtuhumu kujihusisha na kashfa za rushwa, Agosti 29, 2015. REUTERS/Athit Perawongmetha
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya waandamanaji wakiwa wamevalia tisheti za rangi ya njano kuashiria kuwa ni wanamabadiliko, waliandamana kwa siku ya pili Jumapili Agosti 31, wakishinikiza waziri mkuu Najib kuondolewa madarakani wakimtuhumu kwa kashfa ya rushwa.

Akizungumza na waandamanaji, Mahathir Mohamad, ameomba radhi kwa wananchi kufuatia uamuzi wake wa kumuunga mkono waziri mkuu Najib wakati akiingizwa madarakani, na kwamba sasa, anaungana na wananchi kumtaka aondoke.

Waziri mkuu Najib ametupilia mbali tuhuma za rushwa dhidi yake, ambapo amesema serikali yake haiungi mkono maandamano hayo kwa kuwa kwanza hayakuwa na Kibali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.