Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-UCHAGUZI-HAKI-SIASA

Saudi: wanawake kugombea katika uchaguzi wa manispaa

Saudi Arabia imepiga hatua nyingine Jumapili Agosti 30 kwa kukubali wanawake kugombea katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, uchaguzi wa kwanza kuonekana hautoshi kwa vyama vinavyotaka maendeleo na haukubaliki kwa vyama vya Conservative.

Wanawake 70 katika uchaguzi wa manispaa ni ushindi tosha kwa wanawake kushirikishwa katika taasisi za uongozi nchini Saudi Arabia.
Wanawake 70 katika uchaguzi wa manispaa ni ushindi tosha kwa wanawake kushirikishwa katika taasisi za uongozi nchini Saudi Arabia. REUTERS/Fahad Shadeed
Matangazo ya kibiashara

Wanawake nchini Saudi Arabia wamepwa muda hadi katikati ya mwezi Septemba kusimama kama wagombea katika uchaguzi wa manispaa mwezi Desemba, uchaguzi ambao utakua wa kwanza kwa mawanamke kupewa nafasi ya kugombea na kuweza kupigiwa kura.

zoezi la uandikishaji wa wapiga kura lilianza Agosti 22 katika vituo tofauti na vile vya wanaume.

Katika nchi ya kiislamu yenye msimamo mkali wa kidini, ni sheria kwa wanaume na wanawake kujitenga, huku wanawake wakitakiwa kuvaa nguo zinazoficha maumbile yao kuanzia kichwani hadi miguuni. Wanawake hawawezi kufanya kazi yoyote, kuusafiri au kuwa na pasipoti bila idhini yamsiammizi wa familia kama vile baba au mume. Pia ni marufuku kwa wanawake kuendesha gari.

Hayati Mfalme Abdullah, hata hivyo, aliamua mwaka 2011 kuruhusu wanawake kupiga kura na kusimama kama wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2015, akisema wakati huo "kukataa kuwatenga wanawake katika jamii ya Kisaudi."

Mwezi Februari mwaka 2013, mfalme huyo alitoa idadi ya viti maalum kwa wanawake katika baraza la kitaifa la Ushauri, akiwateua wanawake 30 kati ya wajumbe 150 wanaounda baraza hilo.

Haijafahamika iwapo Mfalme Salmane aliyeshika hatamu ya uongozi wa nchi mwezi Januari ataendelea na mpango alioanzisha mtangulizi wake, ambaye ni ngudu yake hayati mfalme Abdallah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.