Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Viongozi wa Afghanistan watangaza kifo cha mullah Omar

Viongozi wa Afghanistan wametangaza Jumatano wiki hii kifo cha mullah Omar, kiongozi mkuu wa kundi la Taliban, aliyekuwa mafichoni tangu mwaka 2001. Tangu kuanguka kwa utawala wa Taliban, uvumi wa kifo cha mullah Omar ulizagazwa mara kadhaa.

Mullah Omar, kiongozi mkuu wa Taliban, akizungukwa na askari wake, mwaka 1996.
Mullah Omar, kiongozi mkuu wa Taliban, akizungukwa na askari wake, mwaka 1996. AFP PHOTO / BBC TV / BBC NEWSNIGHT / FILES
Matangazo ya kibiashara

Mullah Omar, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, alikimbilia katika nchi jirani ya Pakistan baada ya kuanguka kwa utawala wake.

Kiongozi mkuu wa Taliban, anayetambuliwa kwa picha za zamani kutokana na ndevu zake, kilemba chake na jicho lake moja, anakisiwa kufariki dunia miaka miwili iliopita katika hospitali ya Pakistan. Lakini kumekea na mashaka kuhusu kifo chake.

Kiongozi huyo mkuu wa Taliban alionekana mara ya mwisho hadharani mwaka 2001. Mwaka ambao Marekani iliingilia kijeshi nchini Afghanistan kufuatia mashambulizi ya Septemba 11. Katika kipindi cha miaka kumi na nne iliopita, kifo cha mullah Omar kilitajwa mara kadhaa, na juma lililopita uvumi ulizagazwa kuhusu kifo cha kiongozi huyo mkuu wa Taliban.

Mazingira ya kifo chake bado yanatatanisha

Jumatano jioni wiki hii, maofisa wa usalama wa Afghanistan wamesema kuwa Mullah Omar alifariki. Rais wa Afghanistan alithibitisha taarifa hiyo kwa kutoa tangazo rasmi. Mullah Omar aliyetawala nchi katika utawala wa kiimla kati ya mwaka 1996 na 2001, kwa jina la Amiri wa Waumini, anakisiwa kweli kuuawa.

Hata hivyo mazingira ya kifo chake bado yanatatanishai. Katika suala hili, hakuna kilicho rasmi wakati huu. Afisa mwandamizi pekee wa Afghanistan amezungumza kwa masharti ya kutotajwa: Mullah anasadikiwa kufariki dunia nchini Pakistan kufuatia ugonjwa. Inakisiwa pia kuwa alirejeshwa nchini Afghanistan ikwa mazishi.

Muili wake utazikwa kusini mwa nchi, katika mkoa alikozaliwa. Kundi la Taliban halijathibitisha wala kukanusha kifo cha Mullah Omar.

Marekani ina “uhakika” na taarifa ya kifo cha Mullah Omar

Kwa upande wake, Ikulu ya Marekani imebaini kwamba taarifa kuhusu kifo cha Mullah Omar ni yenye "kuaminika" lakini msemaji wa Obama hakutoa maelezo yoyote kuhusu uchunguzi ambao umeanzishwa au tangu wakati Wamarekani walipewa taarifa ya kifo cha mtu huyo aliye kuwa mshirika wa karibu na Osama Bin Laden.

Idara ya upelelezi ya Afghanistan inashirikiana kwa karibu na Wamarekani, ambapo idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan imeanza kupunguzwa. Na mazungumzo yalioanzishwa kati ya viongozi wa Afghanistan na Taliban, ikiwa ni pamoja na Mullah Omar ambaye alikuwa kiongozi, yalikua yakijadiliwa nchini Marekani na kupitishwa wakati wa ziara rasmi ya rais Ashraf Ghani mapema mwaka huu.

Kiongozi mkuu wa Taliban, anayetambuliwa kwa picha za zamani kutokana na ndevu zake, kilemba chake na jicho lake moja, hapa ni kwenye picha ya zamani isiokuwa na tarehe.
Kiongozi mkuu wa Taliban, anayetambuliwa kwa picha za zamani kutokana na ndevu zake, kilemba chake na jicho lake moja, hapa ni kwenye picha ya zamani isiokuwa na tarehe. REUTERS/National Counterterrorism Center

■ Kitita cha dola milioni 10 kilitengwa kwa ajili ya kukamata ya Mullah Omar

Marekani ilitenga kitita cha dola milioni 10 kwa ajili ya kukamata ya mtu aliye kuwa akiongoza Afghanistan kuanzia mwaka 1996 hadi 2001. Mwezi Aprili, Taliban ilichapisha katika mdandao wake wa intaneti wasifu kwa utukufu wa kiongozi wao wa kiroho. Na Julai 15, ujumbe wa Mullah mwenyewe ulikuja kukazia mazungumzo kati ya Serikali ya Ashraf Ghani na Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.