Pata taarifa kuu
Jerusalem-Israeli- Palestina-Usalama

Palestina: Israeli: watu wanne wauawa katika shambulio Jerusalem

Wayahudi wanne raia wa Israeli wameuawa wakiwa wanaswali katika Sinagogi la eneo la wakristo wenye itikadi kali katika kitongoji cha Har Nof, Jerusalem Magharibi.

Wayahudi wanne wauawa katika shambulio lililotekelezwa na Wapalestina wawili ndani ya Msikiti katika kitongoji cha Har Nof, Jerusalem Magharibi, Jumanne Novemba 18 mwaka 2014.
Wayahudi wanne wauawa katika shambulio lililotekelezwa na Wapalestina wawili ndani ya Msikiti katika kitongoji cha Har Nof, Jerusalem Magharibi, Jumanne Novemba 18 mwaka 2014. REUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Inaarifiwa kua Wayahaudi hao wameuawa na raia wawili wa Palestina. Watu sita wakiwemo askari polisi wawili wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Kwa mujibu wa polisi, raia hao wa Palestina ambao pia wameuawa, walishambulia Sinagogi hilo wakitokea Jerusalem Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, washambuliaji hao waliingia mapema ndani ya Sinagogi la eneo linalokaliwa na wakristo wenye itikadi kali jerusalem Magharibi na kuanza kuwashambulia Wayahudi hao..

Inasadikiwa kua raia hao wa Palestina walioendesha shambulio hilo, walikua wamebebelea shoka na visu. Kwa mujibu wa Polisi Wayahudi wanne pamoja na Wapalestina wawili (waliyoshambulia) wameuawa, na watu wengine wengi wamejeruhiwa.

Kundi la Hamas na Islamic Jihad wamepongeza shambulio hilo, ambalo linatokea wakati kukishuhudiwa hali ya wasiwasi, baada ya mfululizo wa makabiliano hivi karibuni karibu na Msikiti wa Al-Aqsa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.