Pata taarifa kuu
SYRIA-IRAQI-ISIL-KOBANE-Usalama

Syria: vikosi vya Kikurdi vyaendelea kufanikiwa Kobane

Wapiganaji wa Dola la Kiislam wanaendelea kuzingira mji wa Kobane tangu miezi miwili iliyopita, wakati ambapo mapigano kati ya wapiganaji hao na wapiganaji wa kikurdi wa Kobane wakisaidiwa na wapiganaji wa Kikurdi kutoka Iraq yamesababisha vifo kutoka pande zote husika katika vita hivyo.

Wapiganaji wa Kikurdi wakikabiliana na wapiganaji wa Dola la Kiislam magharibi mwa Ukraine, Novemba 4 mwaka 2014.
Wapiganaji wa Kikurdi wakikabiliana na wapiganaji wa Dola la Kiislam magharibi mwa Ukraine, Novemba 4 mwaka 2014. REUTERS/Yannis Behrakis
Matangazo ya kibiashara

Tangu wapiganaji wa Kikurdi wa kobane kupata msaada kutoka kwa wapiganaji wa Kikurdi kutoka Iraq, wameendelea kupata mafanikio katika mji wa Kobane, bila hata hivo kufaulu kuwatimua wapiganaji wa dola la Kiislam. Jumatano Novemba 12 wapiganaji hao wa Kikurdi wa Kobane walifankiwa kudhibiti baadhi ya maebeo ya mji huo.

Mapigano hayo kati ya wapiganaji wa Dola la Kiislam na wapiganaji wa Kikurdi katika mji wa Kobane hayatakoma iwapo wapiganaji wa Dola la Kiislam hawatatimuliwa katika maeneo ya mji wa Kobane waliyo yadhibiti.

Wapiganaji wa Kikurdi wa Kobane wakishirikiana na wapiganaji wa Kikurdi kutoka Iraq na syria wamekidhibiti tangu Jumatano novemba 12 kijiji cha Mistanour kusini mashariki mwa mji wa Kobane. Kijiji hicho kwa kipindi cha mwezi moja na nusu kilikua chini ya udhibiti wa wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Hata hivyo wapiganaji hao wa Kikurdi wamekua wakidhibiti kwa siku baadhi ya maeneo ya vijiji viliyo pembezuni mwa mji wa Kobane. Pande zote zimeendelea kupoteza wapiganji katika maeneo mbalimbali ya mji wa Kobane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.