Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-Siasa-Usalama

Israel: Fatah wito kwa "siku ya hasira"

Msikiti wa Al Aqsa uliyokua umefungwa na serikali ya Israel hatimaye umefunguliwa Ijumaa asubuhi Oktoba 31.

Raia wa Palestina akiwa mbele ya gari iliyochomwa na wapinzani mashariki mwa mji wa Jerusalem, Oktoba 30 mwaka 2014.
Raia wa Palestina akiwa mbele ya gari iliyochomwa na wapinzani mashariki mwa mji wa Jerusalem, Oktoba 30 mwaka 2014. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Israel ilichukua uamzi wa kufunga Msikiti huo mtakatifu baada ya shambulio dhidi ya raia mmoja wa Kiyahudi na kifo cha raia mmoja wa Palestina. Lakini msikiti huo umefunguliwa kwa masharti. Wanaume na wanawake waliyo na umri wa miaka zaidi ya 50 ndio wametakiwa kuswali ndani ya Msikiti huo.

Hali ya utulivu imerejea tangu Ijumaa asubuhi Oktoba 31katika mji wa Jerusalem. Wanaume na wanawake walio na umri zaidi ya 50 ndio wametakiwa kushiriki katika sala ya Ijumaa ndani ya Msikiti Al-Aqsa, ambao ni sehemu ya tatu takatifu kwa Waislam.

Hatua hiyo inakuja baada ya Msikiti huo kufungwa moja kwa moja kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa vita vya mawe (Intifada) miaka 14 iliyopita.

Fatah imetangaza Ijumaa Oktoba 31 "siku ya hasira" na polisi ya Jerusalem imeongeza idadi ya askari polisi. Karibu askari polisi 3000 wakiwemo walinzi wa mipaka wametumwa hasa pembezuni mwa mji huo wa zamani. Mkuu wa polisi katika mji huo wa Jerusalem amezitolea wito pande zote husika kuwa watulivu. Katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, kulitokea matukio kadhaa madogo. Vijana wa Kipalestina waliokua wakirusha mawe pamoja na raia wa Kiyahudi wenye msimamo mkali ambao walikua wakijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya Msikiti Al Aqsa walikamatwa...

Yehuda Glick, raia wa Israel aliye shambuliwa Jumatano jioni Oktoba 29 bado amelazwa hospitalini akiwa katika hali ya mautiuti. Moutaz Hijazi anaye daiwa kutekeleza mashambulizi hayo alizikwa Alhamisi usiku Oktoba 30 baada ya kupigwa risasi na vikosi maalumu vya Israel nyumbani kwake. Watu 45 tu ndio waliruhusiwa kuhudhuria mazishi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.