Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI-IRAQ-ISIL-KOBANE-Usalama

Syria: wakurdi wa Kobane wasubiri msaada kutoka kwa ndugu zao wa Iraq

Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria (SOHR) limeeleza kwamba wapiganaji 30 wa Dola la Kiislam pamoja na wapiganaji wa Kikurdi 11 wameuawa Jumanne Oktoba 21katika mapigano yaliyotokea katika mji wa Kobane nchini Syria.

Raia wa Kikudi wakiangalia ndege za kivita zikiwa kwenye anga ya mji wa Kobane.
Raia wa Kikudi wakiangalia ndege za kivita zikiwa kwenye anga ya mji wa Kobane. AFP PHOTO/BULENT KILIC
Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo kundi la wapiganaji wa Kikurdi linaendeendelea kusubiri ndugu zao wa Iraq ambo walaarifiwa tangu usiku wa jumanee kuamkia Jumatatu Oktoba 20 kwamba wanakuja kuwaunga mkono katika vita vyao dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Awali iliarifiwa kwamba wapiganaji wa Kikurdi wa Iraq (Pershmegas) watapitia nchini Uturuki kabala ya kuingia katika mji wa Kobane kuwasaidia kijeshi ndugu zao wa Kikurdi katika vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, lakini mpaka sasa wapiganaji hao hawajaonekana wala hawajawasili katika mji wa Kobane.

Mpaka sasa hali hiyo imezua waswasi, baada ya serikali ya Uturuki kutangaza kwamba imewaruhusu wapiganaji wa Kikurdi wa Iraq kutumia ardhi yake kwa kuingia katika mji wa Kobane.

Vyombo vya habari vya Uturuki vimekua vikijiuliza maswali mengi kuhusu wapiganaji hao, baada ya serikali ya Uturuki kutoa tangazo hilo.

hayoya kijiri viongozi wa Kikurdi katika mji wa Kobane wamekanusha taarifa kwamba wamekuwa wakiwasiliana kwa simu na viongozi wa serikali ya Uturuki, wakati ambapo, Waziri mkuu wa Uturuki, Davutoglu, ameeleza kwamba mazungumzo kati ya serikali ya Uturuki na Wakurdi yanaendelea.

Wakurdi wamekua wakiinyooshea mkono wa lawama serikali ya Uturuki kwamba haina utashi wa kusaidi ili mji wa Kobane usianguki mikononi mwa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Hata hivyo kumekuwa na taarifa kwamba silaha zilizo pewa waasi wa Kikurdi zimeanguka mikononi mwa wapiganaji  wa Dola la Kiisla, baada ya mkanda wa video kuwekwa mtandaonimkasa huo.

Marekani inasema hiyo ni propanga ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam na kwamba wanachunguza kuhusu ukweli wa mkanda huo wa video.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.