Pata taarifa kuu
UINGEREZA - AFGHANISTANI

David Cameron kiongozi wa kwanza barani Ulaya kukutana na rais mpya wa afghanistan Ashraf Ghani

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amekuwa kiongozi wa kwanza wa dunia kukutana na rais mpwa wa Afganistan Ashraf Ghani. Cameron aliwasili jijini Kabul bila kutarajiwa siku ya Ijumaa baada ya kuwatembelea wanajeshi wa Uingereza nchini Cyprus kuzindua mashambuliz ya angaa dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu nchini Iraq na Syria.

David cameron na Ashraf Ghani
David cameron na Ashraf Ghani
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu huyo amesema Uingereza ambayo ina wanajeshi wake zaidi ya elfu katika muungano wa Majeshi ya NATO itaendelea kusimama na Afganistan hata baada ya NATO kuodoka nchini humo mwisho wa mwaka huu.

akiwa nchini Afghanistan, David Camaeron amesema kwa pmoja wamefaulu kuifanya afghanistan na Uingereza salama. na kuongeza kwamba bila shaka serikali ya Umoja wa kitaifa itakabiliana na changamoto nyingi lakini rais Ghani na waziri mkuu Abdullah abdullah wameonyesha jitihada za kuijenga Afghanistan iliyo bora na kuahidi kuwa mshirika wa karibu na rafiki mwema.

Naye rais Ghani amesisitiza umuhimu wa dunia kuendelea kuisaidia Afganistan kuendelea kupambana na wangambo wa Taliban. Ameendelea kuwa wanakabiliana na vitisho vya pamoja, vitisho kwa Uingereza na Marekani, na hili haliepukiki kwani kuna wazuri na wabaya.

Rais Ghani aliapishwa kuwa rais mpya wa Afganistan siku ya Jumatatu, na atahudumu katika serikali ya mpito na Abdulla Abdullah ambaye atasimamia maswala ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.