Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAELI-MISRI-HAMAS-Usalama

Palestina : Gaza :Hamas yapoteza viongozi wake watatu wa kijeshi 

Viongozi watatu wakuu wa kijeshi wa Hamas nchini Palestina wameuawa mapema alhamisi asubuhi wiki hii katika mashambulizio ya anga yaliyoendeshwa na jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza, Hamas imethibitisha.

Jeshi la Israeli linaendelea na mashambulizi ya anga katika ukanda wa Gaza, baada ya siku kadhaa za kusitishwa kwa mapigano.
Jeshi la Israeli linaendelea na mashambulizi ya anga katika ukanda wa Gaza, baada ya siku kadhaa za kusitishwa kwa mapigano. REUTERS/Mohammed Salem
Matangazo ya kibiashara

Tawi la kijeshi la Hamas, Ezzedine al-Qassam, katika tangazo lake limesema limekagua miili hiyo na kubaini kwamba Mohammed Abou Chamala, Raëd al-Atar pamoja na Mohammed Barhoum, ambao ni viongozi wakuu wa kijeshi wa Hamas wameuawa.

Mohammed Abou Chamala na Raëd al-Atar walikua viongozi wakuu wa kijeshi wa tawi la kijeshi la Hamas la Ezzedine al-Qassam, kulingana na taarifa ziliyotolea na chanzo cha Palestina. Abou Chamala alikua kiongozi wa kundi la Al-Qassam, ambalo linaendesha harakati zake kusini mwa ukanda wa Gaza.

Mashambulizi hayo yanatokea siku moja baada ya shambulizi lingine kutokea, ambalo limesababisha vifo vya mke na mtoto wa kiongozi wa kijeshi wa tawi la kijeshi la al qassam, Mohammed Deif, ambaye bado yuko hai, kwa mujibu wa Hamas.

Kwa mujibu wa idara za huduma za dharura, mashambulizi ya anga ya jeshi la Israeli yaliteketeza jengo moja katika mji wa Rafah na kuua watu saba. Haijabainika iwapo viongozi hao watatu wa kijeshi ni miongoni mwa watu hao saba waliyouawa.

Hata hivo, watu wawili akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka 13 wameuawa kaskazini mwa ukanda wa Gaza, huku mtu mwengine akiuawa katika mashambulizi ya jeshi la anga la Israel dhdi ya kambi ya wakimbizi ya Nousseirat.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.