Pata taarifa kuu
PALESTINA-HAMAS-FATAH- Makubaliano

Hamas na Fatah wakubaliana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa

Pande mbili hasimu nchini Palestina Fatah na Hamas hatimaye wameamua kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kuishawishi serikali ya Israeli, wakati ambapo mchakato wa amani umefifia moja kwa moja.

Kiongozi wa Hamas akiwa katika mazungumzo na kiongozi wa Fatah, mjini Gaza aprili 22 mwaka 2014.
Kiongozi wa Hamas akiwa katika mazungumzo na kiongozi wa Fatah, mjini Gaza aprili 22 mwaka 2014. REUTERS/Mohammed Salem
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa chama cha ukombozi wa Palestine cha Fatah na ule wa kundi la Hamas linaloongoza ukanda wa Gaza wameafikiana “kuunda serikali ya umoja wa kitaifa mnamo majuma matano”.

Serikali hio itawashirikisha wajumbe kutoka pande zote, wakiwemo wajumbe kutoka chama cha PLO cha Mahmoud Abbas na kundi la Hamas, amethibitisha mmoja kati ya wajumbe wa chama cha PLO jana jioni alipoifanya ziara katika ukanda wa Gaza .

Kiongozi mkuu wa chama cha Hamas Moussa Abu Marzouk (kushoto) kiongozi mkuu wa chama cha Fatah Azzam Al-Ahmed (wapili kushoto) kiongozi wa serikali ya hamas Ismail Haniyeh (watatu kushoto) naibu spika  wa Bunge la Palestina  Ahmed Bahar
Kiongozi mkuu wa chama cha Hamas Moussa Abu Marzouk (kushoto) kiongozi mkuu wa chama cha Fatah Azzam Al-Ahmed (wapili kushoto) kiongozi wa serikali ya hamas Ismail Haniyeh (watatu kushoto) naibu spika wa Bunge la Palestina Ahmed Bahar REUTERS/Mohammed Salem

Ujumbe wa PLO ulikua unaongozwa na Azzam al-Ahmad, kiongozi wa Fatah, chama kinachoongozwa na rais wa mamlaka ya wapalestina Mahmoud Abbas.

Ujumbe huo ulipokelewa kwa nderembo na vifijo na kiongozi wa serikali ya Hamas katika ukanda wa Gaza, Ismaïl Haniyeh, na mmoja wa vigogo wa chama hicho, Moussa Abou Marzouq.

Pande hizo mbili zimeendelea na mazungumzo leo jumatano asubuhi katika hali ya kuelewana, habari hii ni kwa mujibu wa duru ziliyo karibu na mazungumzo hayo. Mkutano na waandishi wa habari unatarajiwa leo.

Mazungumzo hayo yanahusu uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa, kuandaa kalenda ya uchaguzi mkuu, na marekebisho katika uongozi wa PLO.

Lakini si kwa mara ya kwanza pande hizo hasimu zinafikia makubaliano ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa, ziliafikiakana mara kadhaa, lakini kauli hazikuendana na vitendo.

Kundi hili la Hamas na chama chaFatah walisaini makubaliano ya kuboresha maridhiano ili kukomesha mgawanyiko wa kisiasa kati ya ukingo wa Gaza na Cisjordanie. Lakini makubaliano hayo hayakutekelezwa.

Kundi la Hamas baada ya kushinda uchaguzi mwaka 2006, liliamua kulkifukuza mwaka uliyofuatia chama cha Fatah katika ukanda wa Gaza.

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amemtuhumu leo jumatano rais wa malaka ya wapelestina Mahmoud Abbas kwa kuvunja mchakato wa amani.

“Abu Mazen (jina lingine la Mahmoud Abbas) ameamua kushirikiana na Hamas kwa kutafuta amani kuliko kutafuta amani na Israeli, amesema akisikitika Netanyahu, kulingana na tangazo liliyotolewa na ofisi yake, wakati alipokua akimpokea kwa mazungumzo waziri wa mambo ya nje wa Austria, Sebastian Kurz.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.