Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Mwaka mmoja wa mapigano nchini Sudan kati ya jeshi la serikali na RSF
Wiki hii, ilikuwa ni mwaka mmoja wa vita nchini Sudan, kati ya jeshi la taifa chini ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wa RSF wanaongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo.17/04/202409:34 -
Uhusiano kati ya Somalia na Ethiopia waendelea kuingia baridi
Wiki iliyopita, Somalia ilimfukuza nchini mwake Balozi wa Ethiopia Mukhtar Mohamed kwa madai kuwa nchi hiyo inaingilia mambo yake ya ndani.Mwezi Januari, mzozo wa kidiplomasia ulianza kushuhudiwa nchini humo baada ya Ethiopia kuingia kwenye makubaliano na jimbo la Somaliland, kutafuta njia ya kufika baharini na kujenga kambi ya jeshi kwenye ukanda wake wa pwani.Nini hatima ya mvutano huu ?10/04/202409:21 -
Maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ,ulimwengu umejifunza nini?
Kumbikizi ya miaka 30 tangu mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu hadi laki 8 ,kuna wito wa ulimwengu kuhakikisha watuhumiwa zaidi kusakwa na mataifa yaweke mikakati kuzuia mauaji kama haya kutojirudia03/04/202409:48 -
Raia wa Senegal wamchagua Faye kuwa rais wao mpya
Bassirou Diomaye Faye amechaguliwa kuwa rais mpya wa Senegal.Faye mwenye umri wa miaka 44, mshirika wa karibu wa mwanasiasa mwenye ushawishi Ousamane Sonko, ameahidi kufungua ukura mpya wa uongozi wa nchi hiyo.Kwanini raia wa Senegal wamemchagua Faye ? Tunachambua pamoja na Mali Ali akiwa jijini Paris, na Lutege Musa Lutege akiwa jijini Dar es salaam.27/03/202410:15 -
Makala haya yanatupia jicho uchaguzi wa urais nchini Urusi, nini maana ya ushindi wa rais Vladimir Putin.
20/03/202410:04 -
Burundi: Mgawanyiko kwenye chama kikuu cha upinzani CNL
Nchini Burundi, chama kikuu cha upinzani cha CNL kinashuhudia mgawanyiko baada ya kiongozi wake Agathon Rwasa kuondolewa kwenye nafasi kiongozi wa chama.Hii ilitokea wakati Rwasa akiwa ziarani nchini Kenya.Nini hatima ya kisiasa ya Rwasa ?Tunazungumza naye lakini pia Mali Ali mchambuzi wa siasa za Burundi akiwa jijini Paris.13/03/202410:22 -
Kenya: Kutuma polisi wake nchini Haiti kuthibiti magenge ya wahalifu
Serikali ya Kenya na Haiti zimetiliana saini ili kufanikisha Kenya kutuma polisi wake nchini Haiti kudhibiti magenge ya wahalifu ambayo yameendelea kutatiza usalama nchini Haiti.08/03/202409:59 -
Uongozi wa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir katika jumuiya ya Afrika Mashariki
Rais Salva Kiir amekuwa ziarani Rwanda na Burundi kuangazia swala la usalama28/02/202410:14 -
AU yakosa kupata suluhu kwa mizozo ya Africa
Viongozi wa Africa wamekutana mwisho wa juma katika mkutano wao wa kila mwaka wa 37, nchini Ethiopia walishindwa kuja na njia ya mapoja kumaliza migogoro barani.21/02/202410:02 -
Wabunge nchini Tanzania wapitisha mageuzi ya sheria za uchaguzi
Wiki iliyopita, wabunge nchini Tanzania, walipitisha miswada mitatu ya sheria ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao. Tume ya uchaguzi itabadilishwa jina na sasa itafahamika kama Tume huru ya taifa ya Uchaguzi. Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake, watateuliwa na rais baada ya kupokea majina matatu kutoka kwenye Kamati ya usaili.Chama kikuu cha upinzani, CHADEMA kinapinga mabadiliko hayo.07/02/202409:40 -
Niger, Mali na Burkina Faso kujiondoa ndani ya ECOWAS
Mataifa ya Mali, Niger na Burkina Faso, yametangaza kujiondoa kwenye muungano wa ECOWAS, baada ya vikwazo ambayo muungano huu ulitangaza dhidi ya mataifa hayo, kipindi baada ya mapinduzi ya kijeshi.03/02/202409:42 -
Matarajio ya wakongo baada ya kuapishwa kwa rais Félix Tshisekedi
Wimbi la siasa imeangazia fursa iliyopo kidiplomasia kwa rais wa DRC Felix Thisekedi aliyeapishwa Jumamosi iliyopita, kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili.DR Congo, imekuwa kwenye mvutano wa kidiplomasia na Rwanda, kwa madai kuwa Kigali inawaunga mkono waasi wa M23 eneo la mashariki. Ruben Lukumbuka amewaalika Francois Alwende, mtaalamu wa siasa za DRC akiwa jijini Nairobi pia Guerschome Kahebe pia ni mchambuzi wa siasa akiwa Jijini Washington nchini Marekani.24/01/202410:11 -
Mvutano kati ya ofisi ya rais nchini Kenya na idara ya mahakama
Rais wa Kenya William Ruto, ameingia kwenye mvutano na idara ya Mahakama. Ruto anasema Mahakama imejawa na Majaji mafisadi, wanaopindisha haki na kukwamisha miradi za serikali. Jaji Mkuu Martha Koome amekanusha madai hayo. Nini hatima ya mvutano huu ?17/01/202410:04 -
Mkataba kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland, kizungumkuti
Makala hii imejadili hatua ya rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud kusaini sheria ya kufuta makubaliano kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland, hii ikiashiria kutoridhishwa na matumizi ya bandari ya Berbera, uamuzi unaoibua hofu ya kutokea mgogoro baina ya pande hizo mbili.Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ameangazia hili pamoja na mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Washington Marekani, Abdullahi Boru pamoja na profesa Macharia Munene ni mchambuzi wa siasa, na mtaalamu wa maswala ya kidiplomasia akiwa Jijini Nairobi hapa Kenya10/01/202410:01 -
Utendakazi wa CENI na mrengo wa upinzani katika uchaguzi wa Disemba 20
Maandamano yaliotishwa na upinzani kupinga utendakazi wa CENI yalizimwa na polisi nchini DRC05/01/202410:01
Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa