Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Mkuu wa majeshi ya Kenya Francis Ogolla aaga dunia, ziara ya wajumbe wa EU DRC
Makala hii inaangazia yaliyojiri nchini Kenya na kifo cha mkuu wa majeshi ya nchi hiyo KDF aliyepoteza maisha na maafdisa wengine tisa wa jeshi katika ajali ya helikopta Alhamisi Aprili 18, rais William Ruto alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, mgomo wa wafanyabiashara huko Kampala Uganda, ziara ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa na EU huko Goma kutathmini hali ya kibinadamu kwa waliokimbia mapigano ya M23, Senegal, pia Togo kuhusu ziara ya ujumbe wa ECOWAS, lakini pia mashambulio kati ya Iran na Israel.20/04/202420:07 -
Miaka 30 ya mauaji ya kimbari Rwanda, UN yaondoa jeshi lake DRC na mengineyo duniani
Makala yameangazia mambo mengi ikiwemo maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yanaendelea wiki hii, MONUSCO kuanza kuwaondoa wanajeshi wake eneo la mashariki mwa DRC, mgomo wa madaktari nchini Kenya, mwaka mmoja wa mzozo wa Sudani kutimia jumatatu ya aprili 15 na mengineyo duniani. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi13/04/202420:15 -
Maadhimisho ya miaka 30 mauaji ya kimbari nchini Rwanda, uteuzi wa waziri mkuu mpya DRC
Ni makala maalum, kuhusu kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, tunahoji mchakato wa maridhiano umefikia wapi miaka 30 baadaye..... hali iko vipi kwa sasa. na dunia imepata somo gani? Pia kuhusu mauaji hayo, tutarejelea kauli ya Rais Emanuel Macron iliyoonekana kuwa inalenga kutuliza hisia za waathiriwa.Huko DRC uteuzi wa Judith Tuluka Suminwa, mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu. Mahakama nchini Uganda ilitoa uamuzi wake kuhusu sheria dhidi ya ushoga. Kabla ya kwenda Kenya, Sudani..pamoja na Senegal ambako Bassirou DF aliapishwa kuwa rais mpya, tutakwenda Israeli na maeneo mengine duniani.06/04/202420:18 -
Diomaye Faye kuapishwa jumanne kama rais wa Senegal, ziara ya rais wa DRC Mauretania
Rais mteule wa senegal akutana na rais anayemaliza muhula wake Macky Sall, chama kipya cha aliyekuwa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma chazuwiwa kushiriki uchaguzi wa mwezi mei,kamati ya haki za kibinadamu ya umoja wa mataifa, yaitaka Uingereza kuachana na mpango wake wa kuwahamisha wahamiaji kwenda nchini Rwanda, na rais wa DRC Félix Tshisekedi ahitimisha ziara yake huko Mauretania, tutaangazia siasa za Kenya, Tanzania, yaliyojiri huko Israeli na kwengineko duniani.30/03/202420:10 -
Rais Museveni amteua mwanae kuwa mkuu wa majeshi, kifo cha okende kilipangwa
Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Uganda Yoweri Museveni ya kumteua mwanawe kuwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo, mazishi ya mwanasiasa Cherubin Okende, yaliyojiri nchini Rwanda, lakini pia Sudan huko ambako wiki hii Marekani ilisema kuwa ina matumaini mazungumzo ya kumaliza mzozo wa nchi hiyo yatarejea hivi karibuni baada ya mfungo wa Ramadan, uchaguzi wa urais huko Senegal jumapili ya Marchi 24 tumeangazia yaliyojiri huko Israeli na kwengineko duniani. Ungana nami Reuben Lukumbuka23/03/202420:07 -
Kagame akubali kukutana na Tshisekedi, upinzani Burundi wamfukuza rais wake chamani, Ousmane Sonko aachiwa kule Senegal...
Kwenye Makala ya wiki hii tunaangazia hatua ya Rais Kagame kukubali kukutana na mwenzake wa DRC Tshisekedi, pia tutaangalia alivyofukuzwa chamani kiongozi wa chama cha CNL nchini Burundi, Agathon Rwassa, lakini vilevile kilichojadiliwa katika mkutano kati ya marais wa Kenya, Tanzania na Uganda.16/03/202419:59 -
Mashirika ya misaada yatatizika kuhudumia wakimbizi DRC, Ufaransa yahalalisha uaviaji
Hali ya usalama kuendelea kuzorota mashariki mwa DRC baada ya waasi wa M23 kuteka miji kadhaa kama Nyanzale na maeneo jirani, wabunge nchini Uingereza kupinga mpango wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda, uchaguzi wa urais kufanyika marchi 24 nchini Senegal, mpya wa 32 wa jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.09/03/202420:06 -
Kifo cha rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, hali ya usalama DRC na mengineyo
Yaliyojiri wiki hii ni pamoja na kifo cha rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, na kauli za rais Felix Tshisekedi kuwa yuko tayari kwa mazungumzo na rais mwenza wa Rwanda Paul Kagame, ziara ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed nchini Tanzania na pia Kenya, maandamano ya chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania kule Arusha, yaliyojiri nchini Rwanda, kwenye kanda ya Afrika magharibi lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.02/03/202420:11 -
Rais wa DRC F.Tshisekedi kudumisha amani na jirani zake, mazishi ya mwanariadha Kiptum
Makala hii imeangazia kuzorota kwa hali ya usalama pembezoni mwa mji wa Sake DRC,na kauli za rais Felix Tshisekedi mbele ya wanahabari wiki jijini Kinshasa, maandamano ya chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania kule Mbeya, mazishi ya mwanariadha wa Kenya aliyekuwa anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za marathon Kelvin Kiptum, yaliyojiri nchini Rwanda, na pia kwenye kanda ya Afrika magharibi lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.24/02/202420:13 -
Mashambulio mjini Sake mashariki ya DRC, hali ya Kenya, kifo cha mpinzani wa Urusi
Wiki imejaa matukio ya kutamausha kwanza; wanajeshi wawili wa Afrika kusini waliuawa mashariki mwa DRC, kinara wa upinzani wa nchini Kenya Raila Odinga kuwania uwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, maandamano ya wapinzani nchini Tanzania, yaliyojiri Sudani, pia Senegal huko Afrika magharibi, kifo cha mpinzani huko Urusi Alexei Navalyn, shinikizo za kimataifa dhidi ya Israeli ikubali kusitisha vita dhidi ya Hamas,na mengineyo17/02/202420:10 -
Usalama waendelea kuzorota mashariki DRC,UN na hali ya Sudan
Hali ya wasiwasi iliyoshuhudiwa kwenye mji wa Goma, baada ya waasi wa M23 kuonekana kuukaribia mji huo huko mashariki mwa DRC,ziara ya rais wa Poland nchini Kenya na huko Rwanda, kuapishwa kwa rais mpya wa muda nchini Namibia baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hague GeinGhob, yaliyojiri kwenye kanda ya Afrika magharibi pia uteuzi wa baraza jipya la mawaziri nchini Ufaransa, siasa za Marekani na kwengineko duniani10/02/202420:01 -
Watatu wafa katika mlipuko wa gas jijini Nairobi Kenya, M23 waendeleza mapigano DRC
Miongoni ni pamoja na watu watatu wafariki dunia katika mlipuko wa gesi jijini Nairobi nchini Kenya, kundi la waasi wa Uganda wa ADF waendeleza mauaji ya raia wa kawaida nchini DRC,lakini pia yaliyojiri kwenye kanda ya Afrika Mashariki, Afrika magharibi na Mgomo wa wakulima nchini Ufaransa, hali ya Israeli na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.03/02/202420:07 -
Mvutano kati ya Kigali na Bujumbura, mauaji ya watu zaidi ya 10 Mwesso DRC
Yaliyojiri wiki hii inaangazia kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame kwamba ataitetea nchi yake kwa gharama yoyote ile, upinzani nchini Tanzania uliandamana kupinga mabadiliko ya sheria za uchaguzi, mauaji ya watu zaidi ya kumi mjini Mwesso mashariki mwa DRC, uchaguzi visiwani Komoro hali katika ukanda wa Afrika Magharibi lakini pia uchaguzi mdogo huko Marekani,27/01/202420:09 -
Kuapishwa kwa rais Felix Tshisekedi jumamosi, Rwana na UK njia panda bado
Makala hii imeangazia kuhusu kuapishwa rais wa DRC Félix Tshisekedi baada Mahakama ya katiba kuidhinisha ushindi wake katika uchaguzi wa desemba 20, viongozi wa nchi wananchama wa IGAD walikutana jijini Kampala huku wakitoa wito wa kusitishwa mapigano Sudan, waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak na mpango wa kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda.20/01/202420:14 -
Mahakama ya katiba yaidhisha ushindi wa Tshisekedi, Burundi yafunga mpaka na Rwanda
Mahakama ya katiba huko DRC iliidhinisha ushindi wa rais Félix Tshisekedi,rais wa Uganda Yoweri Museveni awatahadharisha waasi wa ADF, Waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak akabiliwa na wakati mgumu kuhusu suala la kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda, yaliyojiri katika ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia uteuzi wa Gabriel Attal kuwa waziri Mkuu wa kwanza kijana nchini Ufaransa, mashambulio ya jeshi la Israeli yawaathiri raia wa kawaida mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.13/01/202420:09
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.