Jukwaa la Michezo
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Mashindano ya barani Afrika mwaka 2023 yakamilika nchini Ghana
Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na Kenya kuongoza chati ya medali Afrika Mashariki katika mashindano ya Afrika, Shirikisho la soka Cameroon yaondoa kashfa ya udanganyifu wa miaka dhidi ya Nathan Doualla, mkurugenzi mwandalizi wa WRC Safari Rally Jim Kahumbura ajiuzulu, droo ya soka mashindano ya Olimpiki na Nottingham Forest kupokonywa alama nne kutofuata sheria wa fedha Uingereza.23/03/202423:52 -
CAF CL: Tp Mazembe, Yanga na Simba wafahamu wapinzani wao wa robo fainali
Karibu katika makala ya jukwaa la michezo, leo tumekuandalia mengi tukianzia na droo ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani afrika, mashindano ya bara afrika pamoja na droo ya robo fainali katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya.16/03/202423:54 -
Ndondi : Anthony Joshua amshinda Francis Ngannou katika raundi ya pili
Karibu katika makala ya jukwaa la michezo leo tunaangazia kushindwa kwa mwana masumbwi Francis Ngannou na Anthony Joshua,kuanza kwa mashindano ya 13 ya bara Afrika nchini Ghana pamoja na Paris Saint Germain kufuzu katika robo fainali michuano ya klabu bingwa barani ulaya.09/03/202424:04 -
Kenya kujenga uwanja mpya kwa ajili ya michuano ya Afcon mwaka 2027
Karibu katika makala ya jukwaa la michezo leo tunaangazia kujengwa kwa uwanja mpya wa michezo nchini kenya, michuano ya klabu bingwa barani afrika pamoja na taifa la ufaransa kukamilisha ujenzi wa kijiji kitakachotumiwa na wanariadha katika michezo ya olimpiki.02/03/202423:51 -
Mashindano ya Tour du Rwanda mwaka 2024 yamekamilika hii leo jijini Kigali
Karibu katika makala jukwaa la michezo, leo hii tunaangazia kukamilika kwa mashindano ya kuendesha baiskeli ya Tour du Rwanda, mashindano ya mchezo ya gofu Magical kenya open pamoja na klabu ya Yanga na Tp Mazembe kufuzu katika hatua ya robo fainali katika michuano ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani afrika.25/02/202422:41 -
Mashindano ya Tour du Rwanda kuanza hapo kesho katika mji wa Kigali
Karibu katika makala ya Jukwaa la michezo, leo tumekuandalia mengi ikiwemo kuanza kwa mashindano ya kuendesha baiskeli ya Tour du Rwanda, mazungumzo ya kipekee na waziri wa michezo nchini Tanzania Damas Ndumbaro pamoja na kupigwa marufuku mechi nne kwa mchezaji wa timu ya taifa ya senegal Kreppin Diatta.17/02/202424:00 -
AFCON 2024 : DRC kucheza dhidi ya Afrika Kusini katika nafasi ya tatu
Miongoni mwa taarifa kuu tutakazozianhazia ni pamoja na fainali ya kombe la mataifa ya bara afrika AFCON kuchezwa hapo kesho mwenyeji Ivory coast wakipambana na Nigeria. Mchezaji wa tenisi nambari moja barani afrika Ons Jabeur kushindwa katika mashindano ya Abu dhabi na fainali ya kombe la mataifa ya bara Asia kuchezwa leo.10/02/202425:01 -
AFCON 2024: DRC na Nigeria zatinga hatua ya nusu fainali
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na taifa la DR Congo pamoja na Nigeria kufuzu kwa hatua ya nusu fainali katika michuano ya kuwania taji la soka kwa mataifa ya bara Afrika. Dereva wa magari ya langalanga Lewis Hamilton kuhamia katika timu ya Ferrari kutoka Mercedes mwaka 2025.03/02/202423:54 -
AFCON 2024: Michuano ya hatua ya 16 bora kuanza
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya hatua ya 16 kuwania taji la soka kwa mataifa ya bara Afrika. Mashindano ya mchezo wa mikono bara Afrika yanayoendelea kule Misri na Aryna Sabalenka kushinda mashindano ya Australian Open kwa upande wa wanawake.27/01/202423:49 -
Mataifa ya Afrika yaendelea kupambana kutafuta taji la AFCON
Tunaendelea kukuletea uchambuzi wa michuano ya soka kuwania ubingwa kwa mataifa ya Afrika, inayoendelea nchini Cote Dvoire. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania, pia zinapambana kuwania taji hilo. Ungana na wachambuzi wetu Jason Sagini, George Ajowi na Jason Sagini akiwa mjini San Pedro.20/01/202423:56 -
Michuano ya AFCON yaanza nchini Cote Dvoire, nani ataibuka mshindi ?
Michuano ya soka kuwania taji la mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON, inaanza leo nchini Cote Dvoire. Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano haya makubwa kurejea kwenye nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40. Kuna timu 24 zinazotafuta ubingwa wa taji hili, ikiwemo Taifa Stars ya Tanzania na Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Afrika Mashariki na Kati. Wachambuzi wetu Paul Nzioki, George Ajowi na Jason Sagini, akiwa Abidjan, wnachambua.13/01/202423:50 -
CAF yaongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa AFCON 2024
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF kuongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa michuano ya AFCON, itakayoanza Januari 13 nchini Cote Dvoire, Bondia wa DRC Martin Bakole aomba mchango wa fedha kushiriki mechi za mkanda wa WBA, matokeo ya Mapinduzi Cup na kombe la Amani visiwani Zanzibar na Brazil yamfuta kazi kocha Fernando Diniz.06/01/202423:56 -
Timu za Afrika zaanza kutangaza vikosi kuelekea AFCON 2024
Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa vikosi vya mwisho vilivyotangazwa na mataifa kadhaa kuelekea AFCON ya mwaka 2023 itakayoanza Januari 13, 2024, raia wa Rwanda Clare Akamanzi ateuliwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa NBA Africa, Guy Bukasa atangazwa kocha mpya wa AS Kigali, rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach atangaza mikakati ya kujumuisha michezo ya kielektroniki e-sports kwenye Olimpiki na kocha Carlo Ancelotti atia saini mkataba mpya klabuni Real Madrid.30/12/202323:54 -
Kenya yaibuka bingwa wa mashindano ya Tong Il Moo Do
Tuliyokuandalia ni pamoja na Kenya kuhifadhi taji lake la Tong Il Moo Do kwa mara ya 11, mkenya Angella Okutoyi ashinda dhahabu mbili kwenye tenisi ya kimataifa ya W25, uchambuzi wa matokeo ya mechi za Klabu bingwa Afrika wiki hii, Man City kutwaa ubingwa wa Kombe la Klabu bingwa Duniani kwa mara ya kwanza na Mahakama ya Ulaya kupinga uamuzi wa FIFA na UEFA kuzuia kuanzishwa kwa Ligi mpya ya Ulaya kuwa kinyume na sheria.23/12/202323:50 -
Mashindano ya Kimataifa ya Tong-Il-Moo-Do yafanyika nchini Kenya
Kenya yaandaa makala ya 11 ya michuano ya kimataifa ya mchezo wa Tong-Il-Moo-Do jijini Mombasa. Uganda ndio washindi wa CECAFA katika mechi za kufuzu kwa michuano ya CAF ya Shule za Afrika. Al Ahly waishinda Al-Ittihad kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu Kisha Paris Saint - Germain yatinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.16/12/202321:01
Jukwaa la Michezo
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.