Gurudumu la Uchumi
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na uma
Shughuli za sekta binafsi na uwekezaji ni vyanzo vikuu ya ukuaji wa uchumi, uzalishaji wa ajira na maendeleo endelevu.Kwa wastani, sekta binafsi inachangia zaidi ya Asilimia 80 ya mapato ya serikali kwa watu wa kipato cha chini na cha kati, kupitia kodi ya kampuni, kodi ya rasilimali na mapato ya kodi kwa wafanyakazi.Sekta hii inazalisha zaidi ya asilimia 90 ya ajira katika nchi zinazoendelea kiuchumi.04/03/202410:00 -
Ukulima wa matunda Kenya na changamoto zake
Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili inaangazia kilimo cha matunda nchini Kenya, na namna wakulima wa nchi hiyo, wameendelea kukumbatia mbinu mpya za kilimo, uvunaji na usindikaji.04/03/202410:00 -
Changamoto za uhamiaji na fursa zake kwa uchumi
Uhamiaji unaweza kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika ikiwa mtu anaweza kutoa mwelekeo bora wa fedha zinazotumwa na wageni kuelekea uwekezaji na ufadhili wa maendeleo katika nchi za Afrika.Diasporas wanachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi zetu ambazo kimsingi ni nchi za asili lakini pia nchi mwenyeji.04/03/202410:04 -
Kuberoshwa kwa huduma ya intaneti Kenya na ilivyochochea ubunifu
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia namna maboreshi ya huduma ya Inteneti nchini Kenya imechochea maendeleo, biashara na ustawi wa watu.04/03/202410:02 -
Mzozo kati ya Kenya na Tanzania kuhusu mashirika yake ya ndege
Msikilizaji, hatimaye nchi ya Tanzania imeondoa zuio ililoweka juma hili kwa ndege za shirika la Kenya KQ, uamuzi iliyokuwa imeuchukua baada ya Nairobi kukataa kutoa kibali kwa ndege za mizigo za shirika la Tanzania kushusha na kupakia kutokea Kenya.Uamuzi huo msikilizaji ulisababisha mawaziri wa pande zote kukutana na Jumanne ya wiki hii wakakubaliana kumaliza tofauti zilizojitokeza na sasa safarai za ndege za Kenya na zile za Tanzania zitaruhusiwa.04/03/202409:57 -
Mustakabali wa Jumuiya mwaka 2024
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia mustakabali wa jumuiya ya Afrika Mashariki kiuchumi kwa mwaka 2024, hasa baada ya athari za uviko 19 za tangu mwaka 2020 na sasa mdororo wa uchumi wa dunia, ambao umesababisha mataifa masikini, ikiwemo ya ukanda kushuhudia kupanda kwa gharama ya maisha.Nimezungumza na Johnson Denge, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa nchini Kenya.04/03/202409:24 -
Matarajio ya Wafanyabiashara kwa mwaka 2024
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, inaangazia namna wafanyabiashara wamejipanga katika mwaka 2024, kuhakikisha biashara zao zinashamiri licha ya changamoto za kiuchumi zinazoikabili dunia kwa sasa. Mwandishi wetuj Victor Moturi, kwa niaba ya mtayarishaji wa makala haya, Emmanuel Makundi, amezungumza na wafanyabiashara nchini Kenya, ambao mwaka uliopita, walilalama kupata changamoto za kifedha na hata upandaji wa bidhaa na kukosekana kwa dola.04/03/202409:35 -
Matarajio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2024
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia mustakabali wa jumuiya ya Afrika Mashariki kiuchumi kwa mwaka 2024, hasa baada ya athari za uviko 19 za tangu mwaka 2020 na sasa mdororo wa uchumi wa dunia, ambao umesababisha mataifa masikini, ikiwemo ya ukanda kushuhudia kupanda kwa gharama ya maisha.Nimezungumza na Johnson Denge, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa nchini Kenya.11/01/202409:24 -
Mkutano wa China na Afrika pamoja na ziara za viongozi nchi za Magharibi barani Afrika
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili inaangazia mkutano wa nchi ya Uchina na viongozi wa Afrika uliofanyika wiki kadhaa zilizopita, pamoja na ziara za viongozi wa nchi za Marekani, Uingereza na Ujermani kwenye nchi za Afrika Mashariki na Magharibi.Ziara zao zinaashiria nini katika muktadha wa kiuchumi? Emmanuel Makundi amezungumza na Profesa Wetengere Kitojo, kuangazia haya kwa kina.02/11/202309:59 -
Kwanini Bostwana imefanikiwa kwenye sekta ya madini ?
Kwenye sehemu yetu ya pili na ya mwisho kuhusu namna nchi ya Bostwana ilivyopiga hatua kwenye sekta ya madini na uchumi wake kwa kutegemea Almasi, tutasikia kutoka kwa wadau mbalimbali akiwemo mwekezaji binafsi Siddarth Gothi , Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo KGK Bostwana, na mchambuzi binafsi wa siasa, Marisa Lourenco, kutoka Afrika Kusini kuhusu mafanikio hayo lakini pia changamoto katika sekta hiyo.25/10/202308:43 -
Fursa za uwekezaji nchini Bostwana kwa nchi za Afrika Mashariki
Kati ya Oktoba 11 hadi 14 mwezi Oktoba, Bostwana iliandaa maonesho ya Kimataifa ya kibiashara jijini Gaborone, yaliyofanyika pembezoni mwa Jukwaa la kwanza wa kibiashara kati ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya.20/10/202309:41 -
IMF, benki ya dunia zaonya kuhusu kudorora kwa uchumi wa mataifa ya Afrika
Ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara, unatarajiwa kupungua kasi mwaka huu, kutokana na kudorora kwa uchumi wa mataifa ya Afrika Kusini, Nigeria na Angola, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia.Ukuaji wa kikanda utapungua hadi 2.5% mwaka 2023 kutoka 3.6% mwaka jana, imesema ripoti hiyo.Mtayarishaji amezungumza na Johnson Denge, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi, kuangazia ripoti hizi kwa kina.11/10/202309:56 -
Viongozi wa dunia wajadili malengo endelevu ya umoja wa Mataifa
Mwezi uliopita, viongozi wa dunia walikutana jijini New York, Marekani katika mkutano wa 78 wa baraza la umoja wa Mataifa, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ikiwemo usalama wa dunia na ukuaji wa uchumi pamoja na mikakati ya kufikia ajenda ya mwaka 2030 na haja ya kuongeza kasi kutekeleza malengo 17 endelevu. Kuzungumzia yaliyojiri, mtayarishaji wa makala haya alimualika Ebenezer Suleiman Mathew Ikomba, balozi wa vijana wa Tanzania kwenye umoja wa Mataifa.05/10/202309:54 -
Tatizo la uhaba wa dola ya Marekani kwenye nchi za Afrika Mashariki
Katika Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, mtayarishaji wa makala haya amezungumza na Profesa Wetengere Kitojo, mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania, ambapo wanaangazia kuhusu tatizo la uhaba wa dola ya Marekani kwenye nchi za Afrika Mashariki.22/09/202309:55 -
Biashara ya madini yaimarika nchini DRC
Wiki hii tunaangazia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako kunaripotiwa ongezeko kubwa la uzalishaji wa madini ya shaba na kobalt katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Takwimu kutoka sekta ya madini, zinaonesha kuwa uzalishaji wa kobalt imeongezeka na kufikia zaidi ya Tani Laki moja, baada ya serikali kuwekeza asilimia 43 ya bajeti yake ya taifa kwenye sekta hiyo.07/09/202309:52
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .