Pata taarifa kuu

Wanawake kutoka katika mataifa yanayo zungumza lugha ya Kifaransa wahitimisha kongamano jijini Kinshasa

Kongamano la Kimataifa la Wanawake kutoka katika mataifa yanayo zungumza lugha ya Kifaransa limemalizika jana mjini Kinshasa kwa washirika kutolewa mapendekezo ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa Jumuiya ya nchi zinazo zungumza lugha ya kifaransa utaofanyika nchini Senegal baadae mwaka huu.

Picha ya pamoja baada ya kuhitimisha Kongamano la kimataifa la nchini zinazo zungumza lugha ya kifaransa jijini Kinshasa
Picha ya pamoja baada ya kuhitimisha Kongamano la kimataifa la nchini zinazo zungumza lugha ya kifaransa jijini Kinshasa rfi
Matangazo ya kibiashara

Washiriki kutoka katika kila kona ya dunia wamewaomba viongozi wa serikali za nchi zinazozungumza Kifaransa kusaidia kukuza zaidi haki za wanawake kwa kuzingatia mahitaji yao ya ushirikiano wa usawa kati ya wanaume na wanawake katika sera zao za utawala.

Washiriki wa kongamano hilo wameiomba Jumuiya ya Kimataifa ya Francophonie kutoa wito kwa vyama na mashirika ya kiraia kuunga mkono serikali zao husika hususan katika sera za kukuza haki za wanawake.

Waziri wa Ufaransa anayehusika na maswala ya Francophonie, Yamina Benguigui ambaye alikuwa mmoja wa wasemaji wakati wa sherehe za kutamatishwa kwa mkutano huo, ameahidi kufanya bidii kujipenyeza popote iwezekanavyo ili kuendeleza haki za wanawake, sanjari na Waziri wa Jinsia nchini DRC, Genevieve Inagosi ambaye amezitaka nchi hizo kubadilishana uzoefu wa kiutendaji katika kukuza jukumu la wanawake hasa katika sekta ya kiuchumi.

Miongoni mwa wanawake waliohudhuria kongamano hilo mjini Kinshasa ni Olive Lembe Kabila, mke wa Rais Joseph Kabila wa DRC, Aminata Maiga, Mke wa rais Ibrahim Boubakar Keita wa Mali, Rais Catherine Samba Panza wa Jamhuri ya Afrika ya kati na Mary Robinson, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kanda ya Maziwa Makuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.