Pata taarifa kuu
Ukraine-mzozo

Serikali ya Urusi imeendelea kutolewa wito wa kuondowa majeshi yake nchini Ukraine, huku ikitishiwa kutengwa na Jumuiya ya Kimataifa

Mataifa ya magharibi yameendelea kuishinikiza serikali ya Urusi kuondowa wanajeshi wake nchini Ukraine na kwamba suluhusu ya mzozo wa taifa hilo utapatikana kupitia mazungumzo. Haya yanajiri wakati huu waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akitishia kuwa Marekani itaweka vikwazo vya kusafiri kwa viongozi wa Urusi, kitisho ambacho Urusi imesema hakina mshiko. 

Majeshi ya Urusi katika ardhi ya Ukraine
Majeshi ya Urusi katika ardhi ya Ukraine
Matangazo ya kibiashara

John Kerry amesema, urusi inatakiwa kufikiria kwa makini kuhusu hatuwa hiyo, na ikumbuke kuna zuio la visa, kuzuiliwa kwa mali, Kutengwa kibiashara pamoja na wafanyabiashara wa Marekani kuanza kufikiria upya ushirikiano wao na Urusi ambayo amesema inaonyesha tabia mbaya.

Viongozi wa Mataifa ya Magharibi wakiongozwa na rais wa Marekani Barrack Obama wameishtumu Urusi kuvamia Ukraine kijeshi na kutishia kusita uhusiano wao na Moscow ikiwa haitawaiondoa wanajeshi wake.

Hayo yanajiri wakati Urusi ikiendelea kutishia kuingilia zaidi kijeshi nchini Ukraine ambapo inaweza kuzuia mzozo mkubwa wa kimataifa ambao itakuwa ni hatari sana kuwahi kutokea tangu kuvunjika kwa muungano wa mataifa ya kikoministi.

Mataifa ya magharibi yanaendeleza shinikizo dhidi ya hatuwa ya Urusi kupeleka vikosi katika ardhi ya Ukraine ambayo itakuwa ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Mataifa hayo yanatishia pia kuiwekea vikwazo Urusi ambavyo miongoni ni kuitenga zaidi.

Vladimir Poutine bado anaendelea kuzua hali ya sintofahamu kufuatia nia yake, lakini katika mawasiliano kwa njia ya sim na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Poutine alikubali kuundwa kwa tume maalum itayo anzisha mazungumzo ya kisiasa nchini Ukraine.

Waziri Mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk anasema taifa lake liko katika hali ya hatari na ameishtumu Urusi kutangaza vita dhidi ya nchi yake. Wanajeshi wa Urusi kwa sasa wanapiga kambi katika mji wa Crimea ambao upo mpakani mwa mataifa hayo mawili na maakazi ya wananchi wa Mataifa yote mawili.

Yatsenyuk anamtaka rais Putin kuamuru wanajeshi wake kurejea katika kambi zao na kuheshimu maafikiano ya Kimataifa kuhusu eneo hilo la Crimea.

Moscow inasema kuwa jeshi lake linawalinda raia wake katika mji huo ambao tayari majengo kadhaa ya serikali yamesimikwa na Bendera ya Urusi.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon amesema atakutana na waziri wa mambo ya mnje wa Urusi hivi karibuni kunshinikiza

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.