Pata taarifa kuu
Bangladesh - ghasia

Taifa la Bngladesh laekea kwenye machafuko baada ya uchaguzi wa jana jumapili kugubikwa na ghasia za mauaji

Bangladeshi inaelekea kutumbukia katika machafuko baada ya uchaguzi wa wabunge ulifanyika jana Jumapili na ambao ulisusiwa na upinzani, huku waziri mkuu wa nchi hiyo akiwatuhumu wapinzani wake kuhusika katika ghasia za hapo jana.

Makabiliano kati ya polisi na wananchi katika mji wa Gaibandha, tarehe 5 Januari
Makabiliano kati ya polisi na wananchi katika mji wa Gaibandha, tarehe 5 Januari REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Sheikh Hasina kiongozi wa serikali amesema upinzani umekosea kususia uchaguzi uliokipa chama chake cha Jumuiya ya Awami ushindi wa asilimia 80 ya kura kufuatia kukosekana kwa upinzani katika uchaguzi ambao umegubikwa na ghasia zilizo gharimu maisha ya watu 26.

Chama kikuu cha upinzani cha BNP kilikuwa kinataka kuwepo kwanza na serikali isioegemea upande wowote kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi huo, jambo ambalo serikali ilitupilia mbali

Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi huo, Sheikh Hasina amesema kususia kwa upinzani kwenye uchaguzi huo hakumaanishi kuwa uchaguzi hauna uhalali wowote hasa kwamba wananchi wengi wameshiriki.

Kiongozi huyo amebaini kwamba kabla ya uchaguzi huo alipendekeza kwa mpinzani wake mkuu Khaleda Zia kushirki katika serikali ya mpito huku wizara kadhaa zikitolewa kwa upinzani kwa ajili ya kuliongoza taifa, mapendekezo ambayo amesema hayakupokelewa.

Sheikh Hasina amesema iwapo upinzani unaokuwa umefanya kosa kubwa sana la kutoshiriki kwenye uchaguzi, hii ni fursa kwao kuonyesha nia ya kuachana na ugaid na kuleta mapendekezo
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.