Pata taarifa kuu
Israeli- Palestina- Wafungwa

Serikali ya Israeli yawaacha huru wafungwa 26 raia wa Palestina katika kutekeleza ahadi zake kuelekea kwenye mazungumzo ya amani

Takriban watu 26 raia wa Palestina waliokuwa wanazuiliwa nchini Israeli, wameachiwa huru, katika mchakato wa kuanzisha mazungumzo ya amani baina ya pande hizo mbili. Hatuwa ambayo imepongezwa na mataifa kadhaa duniani

Kinamama mji Gaza wakimsubiri ndugu yao ambaye ni miongoni mwa walioachwa huru na serikali ya Israeli 30 desemba 2013.
Kinamama mji Gaza wakimsubiri ndugu yao ambaye ni miongoni mwa walioachwa huru na serikali ya Israeli 30 desemba 2013. REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa
Matangazo ya kibiashara

Watu hao 26 walioachwa huru na serikali ya Israeli ni miongoni mwa wafungwa waliozuiliwa kabla ya kufikia kwa mkataba wa jijini Oslo mwaka 1993 na ambao walikuwa wanatuhumiw akwa njia moja ama nyingine katika mauji ya raia wa Israeli.

Mamia ya wananchi wa Ramallah wamejitokeza kwa wingi Ikulu ya rais wa Mamlaka ya wa Palestina kuwalaki ndugu zao waloachwa huru katika Usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne.

wananchi wengi wameonekana kujawa na furaha kufuatia hatuwa hiyo ambayo wengi wamesema ni njia inayoelekea kupatikana kwa amani ya kudumu baina yao na majirani zao wa Israeli

Rais Mahmoud Abbas ametumia fursa hiyo kuitolea wito serikali ya Israeli kuwaachia huru wafungwa wengine wa Palestine wanaokadiriwa kufikia elfu tano na ambao bado wanazuiliwa nchini Israeli.

Kabla ya hatuwa hiyo, takriban waandamaji mia mbili wa Israeli waliandamana kwenye maeneo ya ofisi ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu wakilaani hatuwa ya kuachiwa huru kwa wafungwa watano wa kipalestina kutoka katika eneo la Jerusam mashariki wanaotuhumiwa kupewa vibali vya kueshi katika eneo hilo na viongozi wa Israeli.

Mahakama kuu nchini Israeli hapo jana ilitupilia mbali pengamizi zilizotolewa dhidi ya hatuwa hiyo iliochukuliwa na Israeli baada ya kuahidi mbele ya rais wa Marekani Barack Obama na viongozi wa Palestina katika mchakato wa mazungumzo ya amani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.