Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

UN: Serikali ya Sudan na waasi wa SPLM-N wanakwamisha operesheni ya chanjo ya Polio

media John Ging, mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa, UN Reuters

Serikali ya Sudan na kundi la waasi wa Darfur kwa mara nyingine wamewazuia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwenda kwenye maeneo yenye wakimbizi kwaajili ya kutekeleza operesheni ya chanjo ya polio kwa zaidi ya watoto laki moja na elfu sitini.

Kukataliwa kwa wafanyakazi hao kuingia kwenye maeneo yenye mzozo kunakuja hata licha ya pande hizo mbili kutiliana saini mkataba wa kusitisha vita kwa muda kuruhusu mashirika na kimataifa ya misaada kutoa chanjo ya polio kwa watoto.

Mkuu wa masuala ya misaada ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa UN, John Ging ameeleza kusikitishwa na namna ambavyo Serikali ya Sudan na kundi la waasi wa Sudan People's Liberation Movement-North (SPLM-N) wanavyoendelea kuzuia mashirika ya misaada kufika kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mapigano.

Ging amesema kuwa suala hilo tayari ameliwasilisha kwenye nchi wanachama za baraza la usalama la umoja hupo kuongeza shinikizo kwa Serikali ya Sudan na waasi wa SPLM-N kuacha mara moja tabia ya kuwazuia wafanyakazi wake kutekeleza majukumu muhimu ya kibinaadamu.

Ugonjwa wa Polio umeripotiwa tena kwenye nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo shirika la afya Ulimwenguni WGO limeonya iwapo hatua hazitachukuliwa kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo hali itakuwa mbaya zaidi.

Umoja wa Mataifa UN, umesema kuwa kuna hofu kubwa ya kuenea kwa ugonjwa huo kwenye eneo la Kordofan Kusini na Blue Nile ambako makundi ya waasi yamekuwa yakikabiliana na wanajeshi wa Serikali huku mamia ya watoto wakihitaji msaada wa matibabu na chanjo ya polio.

Umoja wa Mataifa UN ulifanikiwa kuzishawishi pande hizo mbili kutia saini mkataba wa amani November 5 mwaka 2012 lakini toka wakati huo bado kundi la SPLM-N na vikosi vya Serikali wameendelea kukabiliana kwenye maeneo hayo.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana