Pata taarifa kuu
DRC-M23-OXFAM

Oxfam yaonya kuhusu kuzuka kwa mapigano mapya mashariki mwa DRC iwapo makundi mengine ya uasi hayatasalimu amri

Shirika la kimataifa la misaada nchini Uingereza, Oxfam hii leo limeonya kuhusu hali ya amani mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC likitaka kuwepo kwa suluhu ya kisiasa kumaliza machafuko kwenye taifa hilo. 

Sehemu ya wapiganaji toka makundi ya waasi yanayofanya shughuli zao mashariki mwa DRC
Sehemu ya wapiganaji toka makundi ya waasi yanayofanya shughuli zao mashariki mwa DRC Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yake shirika la Oxfam limeonya kuwa huenda amani ya kudumu isipatikane mashariki mwa nchi hiyo kwakuwa si makundi yote ambayo yametangaza kuweka silaha chini na kuacha uasi.

Kwenye ripoti yake, shirika hilo linasema kuwa mashariki mwa DRC kuna zaidi ya makundi 30 ya uasi ambayo yamekuwa yakikabiliana na Serikali ya Kinshasa kutaka kujumuishwa kwenye jeshi la Serikali.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa wananchi wa eneo la mashariki mwa DRC wameendelea kuwa kwenye hali ya hatari kila siku kutokana na kuwepo kwa hatari ya kuzuka kwa mapigano mengine licha ya kundi la M23 kufurushwa kwenye maeneo mengi na kutangaza kucha uasi.

Shirika la Oxfam limetoa wito kwa Serikali ya Kinshasa na vikosi vya Umoja wa Mataifa Un vilivyoko nchini DRC kuchukua hatua mathubuti kuyazibiti makundi mengine ya waasi mashariki mwa nchi hiyo pamoja na kupata suluhu ya kisiasa.

Oxfam inataka makundi mengine ya waasi kusalimisha silaha zao na yale yaliyohusika na ukiukaji wa haki za binadamu viongozi wake wafikishwe kwenye vyombo vya sheria ama sivyo kutarajiwe kushuhudiwa tena kuzuka kwa mapigano mapya na kuongezeka kwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu kunakofanywa na makundi haya.

Taarifa ya Oxfam inatolewa wakati huu ambapo saa chache zijazo ujumbe wa Serikali ya Kinshasa utatiliana saini mkataba wa amani na waasi wa M23 mjini Kampala kumaliza mwaka mmoja na nusu wa mapigano kwenye eneo la mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.