Pata taarifa kuu
CYPRUS-EU-ECB-IMF

Benki nchini Cyprus zaanza kufanya kazi, licha ya maandamano ya wananchi

Benki nchini Cyprus kwa mara ya kwanza hii leo zimeanza kufanya kazi kama kawaida kufuatia kuwa zimefungwa kwa karibu wiki mbili kutokana na mzozo uliokuwepo kati ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya kuhusu kupatiwa mkopo wa Euro bilioni 10 kunusuru uchumi wake.

Wananchi wa Cyprus wakiandamana wakiwa na mabango kukashifu Umoja wa Ulaya na Serikali yao
Wananchi wa Cyprus wakiandamana wakiwa na mabango kukashifu Umoja wa Ulaya na Serikali yao Reuters
Matangazo ya kibiashara

Benki hizo zinafunguliwa wakati wananchi wa taifa hilo wameendelea na maandamano ya kupinga nchi yao kupatiwa mkopo kuinusuru na mdororo wa uchumi ambao iwapo hatua zisingechukuliwa ingeshuhudiwa taifa hilo likifilisika.

Juma hili maelfu ya wananchi wa Cyprus wamefanya maandamano ya nchi nzima wakipinga mpango huo wa Serikali kwa madai kuwa itachangia vijana wengi kukosa ajira jambo ambalo ltachangia kuongezeka kwa uhalifu nchini humo.

Umoja wa Ulaya pamoja na Shirika la Fedha Duniani IMF, waliitaka nchini ya Cyprus kuchukua hatua za kubana matumizi kwa kuhakikisha inadhibitia mfumo wa fedha kwenye benki zake jambo ambali lilisababisha kufungwa kwa benki ya pili kwa ukubwa nchini humo.

Mbali na kuzibana benki, nchi hiyo pia ilitakiwa kutoza riba ya asilimia kumi kwa wananchi ambao wanakiasi cha euro laki moja kwenye akaunti zao huku wengine waliokuwa wamehifadhi kwenye benki ya Laiki wakifilisiwa fedha zao.

Serikali ya Cyprus imesisitiza kuwa ilikuwa ni lazima kuchukua hatua hizo ili kuinusuru nchi hiyo kufilisika na kwamba inafahamu ni kwakiasi gani wananchi wake wataumia moja kwa moja na mpango huo.

Katika mpango huo pia unakataza wasafiri wanaotoka nje ya Cyprus kusafiri na kiasi cha Euro elfu moja na kwamba wanafunzi wa kigeni nchini humo wataruhisiwa kutumia kiasi cha euro elfu 5 kwa mwatumizi ya kawaida.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.