Pata taarifa kuu
CYPRUS-EU-ECB-IMF

Hatimaye nchi ya Cyprus yafikia makubaliano na Umoja wa Ulaya kuhusu kupatiwa mkopo

Nchi ya Cyprus hatimaye imefanikiwa kufikia makubalino kati yake na viongozi wa Umoja wa Ulaya Eu na shirika la fedha duniani IMF kuhusu mpango wa nchi hiyo kupatiwa mkopo wa euro bilioni 10 kunusuru uchumi wake. 

EUTERS/Bogdan Cristel
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo mapya yatashuhudia kufungwa kwa benki ya pili kwa ukubwa nchini humo ya Laiki ambapo fedha zake sasa zitahamishiwa benki kuu ya Cyprus kwa lengo la kudhibiti mzunguko wa fedha.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo ya kina kati ya rais wa Cyprus, Nicos Anastasiades na viongozi wa Benki ya Umoja wa Ulaya, Shirika la Fedha na viongozi wa Umoja wa Ulaya ambao walifikia makubaliano hayo.

Makubaliano hayo pia yatashuhudia watu walio na kiwango cha chini ya euro laki moja kwenye benki ya Laiki wakihamishiwa kwenye benki kuu ya nchi hiyo huku pia benki kuu ikitakiwa kutoza riba zaidi kwa wafanyabiashara wakubwa wa Urusi.

Watu walioathirika kwenye benki la Laiki ambao walikuwa na zaidi ya euro laki moja kwenye akaunti zao watashuhudiwa fedha zao zikizuiliwa na na kuelekezwa kwenye maeneo mengine kupunguza deni la nchi hiyo.

Hatua hiyo inakuja kutokana na sheria ya Umoja wa Ulaya EU ambao haigarantii kiwango hicho cha fedha kuwepo katika benki za ukanda wao.

Kufungwa kwa benki hiyo kumesababisha maelfu ya wafanyakazi wa benki hiyo kukosa ajira kwa sasa jambo ambalo limeibusha hisia kali toka kwa wananchi na wafanyakazi ambao wamepoteza fedha zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.