Pata taarifa kuu
ERITREA

Hali ya utulivu yarejea mjini Asmara, Eritrea baada ya kikundi cha wanajeshi kuteka jengo la wizara ya habari

Hali ya utulivu imerejea mjini Asmara kufuatia siku ya Jumatatu kikundi cha wanajeshi kuteka jengo la wizara ya habari na kituo cha televisheni ya taifa kushinikiza kuachiliwa huru kwa wafungwa wakisiasa wanaoshikiliwa na Serikali. 

Rais wa Eritrea, Issaias Afeworki
Rais wa Eritrea, Issaias Afeworki Reuters
Matangazo ya kibiashara

Utulivu umerejea baada ya wanajeshi hao kuwa na mazungumzo ya muda mrefu na viongozi wa Serikali kuhusu madai yao ambapo wanaelekea kupata muafaka ili kuinusuru nchi hiyo kuingia kwenye machafuko.

Askari zaidi ya miambili walioasi nchini Eritrea wameendelea kushikilia ofisi ya wizara ya habari na baadhi ya ofisi nyingine za Serikali mjini Asmara wakitaka kufanyika mabadiliko ya kidemokrasia.

Licha ya kwamba hakukuwa na makabiliano yoyote ya risasi bado hofu imeendelea kutanda nchini humo ambapo wachambuzi wa mambo wameonya dhidi ya kufanyika mapinduzi nchini humo.

Mara baada ya kuteka majengo ya wizara hiyo wanajeshi hao pia waliteka kituo cha televisheni ya taifa nchini humo na kumuagiza mhariri wake kutoa tangazo kwa Serikali kutaka kuachiliwa huru kwa zaidi ya wafungwa 5000 wa kisiasa wanaoshikiliwa na Serikali.

Nchini hiyo imekuwa ikiongozwa na rais Isaias Afewerki kwa zaidi ya miongo miwili sasa toka ijipatie uhuru wake toka kwa majirani zao Ethiopia baada ya kupigana vita kwa muda mrefu.

Wanajeshi watiifu kwa Serikali walikuwa wamezunguka majengo ya wizara ya habari huku kukiwa na taarifa kuwa huenda ukawa sio mpango wa kutaka kuipindua Serikali bali ni kutaka kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa wanaoshikiliwa na Serikali.

Muwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Eritrea amesema kuwa wanajeshi hao hawajatumia risasi kuwatisha wananchi na kwamba hali ya usalama ni shwari nchini humo licha ya tukio ambalo limetokea na kwamba hali inatarajiwa kurejea kwenye utulivu hizi karibuni.

Katika siku za hivi karibuni jeshi la Eritrea limeshuhudia mgawanyiko mkubwa kufuatia kuibuka makundi yanayoiunga mkono Serikali na wale ambao wanataka kufanyika mabadiliko ya kidemokrasia nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.