Pata taarifa kuu
ICC-SIERRA LEONE-LIBERIA

Mahakama maalumu ya Umoja wa Mataifa kuhusu Sierra Leone, imeanza kusikiliza rufaa ya Charles Tylor

Majaji wa mahakama maalumu ya Umoja wa Mataifa inayosikiliza kesi ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone, hii leo wanasikiliza rufaa iliyowasilishwa na mawakili wanaomtetea rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor wakipinga hukumu ya miaka 50 aliyopewa mteja wao. 

Rais wa zamani wa Liberia, Charles Tylor akiwa kwenye mahakama ya ICC
Rais wa zamani wa Liberia, Charles Tylor akiwa kwenye mahakama ya ICC ICC
Matangazo ya kibiashara

Mwaka 2011 mwezi April mahakama hiyo ya ICC ilimuhukumu kifungo cha miaka 50 jela Charles Taylor baada ya kumkuta na hatia ya kushiriki njama za kupanga mauaji nchini Sierra Leone kwa kuwafadhili waasi kwa silaha akibadilishana na Almasi.

Mbali na kudaiwa kufadhili waasi wa Sierra Leone, Tylor pia anadaiwa kushiriki kupanga mauaji ya halaiki nchini humo kati ya mwaka 1996 na 2002 ambapo watu zaidi ya laki moja na ishirini elfu walipoteza maisha.

Rais huyo wa zamani wa Liberia ameendelea kukana mashtaka yaliowasilishwa mbele yake hata baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo ambapo aliahidi kukata rufaa dhidi ya hukumu ya awali.

Hii leo majaji wa mahakama hiyo wanatarajiwa kuusikiliza upande wa utetezi watakapowasilisha rufaa yao kupinga hukumu ya awali ambapo wanadai kuwa majaji walikosea kwenye hukumu ya awali.

Mawakili wa Tylor wameendelea kusisitiza mteja wa hakutendewa haki wakati wa usikilizwai wa kesi hiyo na kuongeza kuwa hukumu hiyo ilienda kinyume na haki za binadamu.

Rufaa hiyo imevuta hisia za wananchi wa Liberia na Sierra Leone ambao wanataka kiongozi huyo anyongwe kutokana na makosa aliyoyafanya huku wengine wakiona alistahili kifungo cha maisha jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.