Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Rais Museveni amteua mwanae kuwa mkuu wa majeshi, kifo cha okende kilipangwa
Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Uganda Yoweri Museveni ya kumteua mwanawe kuwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo, mazishi ya mwanasiasa Cherubin Okende, yaliyojiri nchini Rwanda, lakini pia Sudan huko ambako wiki hii Marekani ilisema kuwa ina matumaini mazungumzo ya kumaliza mzozo wa nchi hiyo yatarejea hivi karibuni baada ya mfungo wa Ramadan, uchaguzi wa urais huko Senegal jumapili ya Marchi 24 tumeangazia yaliyojiri huko Israeli na kwengineko duniani. Ungana nami Reuben Lukumbuka23/03/202420:07 -
Kagame akubali kukutana na Tshisekedi, upinzani Burundi wamfukuza rais wake chamani, Ousmane Sonko aachiwa kule Senegal...
Kwenye Makala ya wiki hii tunaangazia hatua ya Rais Kagame kukubali kukutana na mwenzake wa DRC Tshisekedi, pia tutaangalia alivyofukuzwa chamani kiongozi wa chama cha CNL nchini Burundi, Agathon Rwassa, lakini vilevile kilichojadiliwa katika mkutano kati ya marais wa Kenya, Tanzania na Uganda.16/03/202419:59 -
Mashirika ya misaada yatatizika kuhudumia wakimbizi DRC, Ufaransa yahalalisha uaviaji
Hali ya usalama kuendelea kuzorota mashariki mwa DRC baada ya waasi wa M23 kuteka miji kadhaa kama Nyanzale na maeneo jirani, wabunge nchini Uingereza kupinga mpango wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda, uchaguzi wa urais kufanyika marchi 24 nchini Senegal, mpya wa 32 wa jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.09/03/202420:06 -
Kifo cha rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, hali ya usalama DRC na mengineyo
Yaliyojiri wiki hii ni pamoja na kifo cha rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, na kauli za rais Felix Tshisekedi kuwa yuko tayari kwa mazungumzo na rais mwenza wa Rwanda Paul Kagame, ziara ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed nchini Tanzania na pia Kenya, maandamano ya chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania kule Arusha, yaliyojiri nchini Rwanda, kwenye kanda ya Afrika magharibi lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.02/03/202420:11 -
Rais wa DRC F.Tshisekedi kudumisha amani na jirani zake, mazishi ya mwanariadha Kiptum
Makala hii imeangazia kuzorota kwa hali ya usalama pembezoni mwa mji wa Sake DRC,na kauli za rais Felix Tshisekedi mbele ya wanahabari wiki jijini Kinshasa, maandamano ya chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania kule Mbeya, mazishi ya mwanariadha wa Kenya aliyekuwa anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za marathon Kelvin Kiptum, yaliyojiri nchini Rwanda, na pia kwenye kanda ya Afrika magharibi lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.24/02/202420:13 -
Mashambulio mjini Sake mashariki ya DRC, hali ya Kenya, kifo cha mpinzani wa Urusi
Wiki imejaa matukio ya kutamausha kwanza; wanajeshi wawili wa Afrika kusini waliuawa mashariki mwa DRC, kinara wa upinzani wa nchini Kenya Raila Odinga kuwania uwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, maandamano ya wapinzani nchini Tanzania, yaliyojiri Sudani, pia Senegal huko Afrika magharibi, kifo cha mpinzani huko Urusi Alexei Navalyn, shinikizo za kimataifa dhidi ya Israeli ikubali kusitisha vita dhidi ya Hamas,na mengineyo17/02/202420:10 -
Usalama waendelea kuzorota mashariki DRC,UN na hali ya Sudan
Hali ya wasiwasi iliyoshuhudiwa kwenye mji wa Goma, baada ya waasi wa M23 kuonekana kuukaribia mji huo huko mashariki mwa DRC,ziara ya rais wa Poland nchini Kenya na huko Rwanda, kuapishwa kwa rais mpya wa muda nchini Namibia baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hague GeinGhob, yaliyojiri kwenye kanda ya Afrika magharibi pia uteuzi wa baraza jipya la mawaziri nchini Ufaransa, siasa za Marekani na kwengineko duniani10/02/202420:01 -
Watatu wafa katika mlipuko wa gas jijini Nairobi Kenya, M23 waendeleza mapigano DRC
Miongoni ni pamoja na watu watatu wafariki dunia katika mlipuko wa gesi jijini Nairobi nchini Kenya, kundi la waasi wa Uganda wa ADF waendeleza mauaji ya raia wa kawaida nchini DRC,lakini pia yaliyojiri kwenye kanda ya Afrika Mashariki, Afrika magharibi na Mgomo wa wakulima nchini Ufaransa, hali ya Israeli na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.03/02/202420:07 -
Mvutano kati ya Kigali na Bujumbura, mauaji ya watu zaidi ya 10 Mwesso DRC
Yaliyojiri wiki hii inaangazia kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame kwamba ataitetea nchi yake kwa gharama yoyote ile, upinzani nchini Tanzania uliandamana kupinga mabadiliko ya sheria za uchaguzi, mauaji ya watu zaidi ya kumi mjini Mwesso mashariki mwa DRC, uchaguzi visiwani Komoro hali katika ukanda wa Afrika Magharibi lakini pia uchaguzi mdogo huko Marekani,27/01/202420:09 -
Kuapishwa kwa rais Felix Tshisekedi jumamosi, Rwana na UK njia panda bado
Makala hii imeangazia kuhusu kuapishwa rais wa DRC Félix Tshisekedi baada Mahakama ya katiba kuidhinisha ushindi wake katika uchaguzi wa desemba 20, viongozi wa nchi wananchama wa IGAD walikutana jijini Kampala huku wakitoa wito wa kusitishwa mapigano Sudan, waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak na mpango wa kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda.20/01/202420:14 -
Mahakama ya katiba yaidhisha ushindi wa Tshisekedi, Burundi yafunga mpaka na Rwanda
Mahakama ya katiba huko DRC iliidhinisha ushindi wa rais Félix Tshisekedi,rais wa Uganda Yoweri Museveni awatahadharisha waasi wa ADF, Waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak akabiliwa na wakati mgumu kuhusu suala la kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda, yaliyojiri katika ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia uteuzi wa Gabriel Attal kuwa waziri Mkuu wa kwanza kijana nchini Ufaransa, mashambulio ya jeshi la Israeli yawaathiri raia wa kawaida mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.13/01/202420:09 -
Dunia yakaribisha mwaka mpya, mvutano kati ya rais Ruto na idara ya mahakama
Miongoni mwa habari kuu za wiki hii ni pamoja na dunia kuukaribisha mwaka mpya 2024, mvutano kati ya rais wa Kenya William Ruto na idara za mahakama, wapinzani wa DRC waendelea kuonesha kutofurahishwa na ushindi wa rais Felix Tshisekedi kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa desemba 20 mwaka uliopita, yaliyotangazwa na CENI, yaliyojiri katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia mashambulio mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.06/01/202420:15 -
DRC: Rais Felix Tshisekedi ashinda uchaguzi kwa muhula wa pili
Baadhi ya habari ambazo tumeangazia ni matokeo ya uchaguzi nchini DRC ambapo Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi kwa muhula wa pili kwa asilimia 73.34, katika matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa na Ceni Jumapili jioni.31/12/202320:01 -
Raia DRC wasubiri matokeo ya uchaguzi, Rais Biden amsuta Netanyahu kulinda raia
Kwenye makala yaliyojiri wiki hii, tumeangazia uchaguzi kule DRC wakati huu shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea, kikosi cha jumuiya ya Afrika Mashariki chaondoka rasmi nchini DRC, mapigano kule Sudan.24/12/202320:01 -
CENI uchaguzi utafanyika desemba 20 DRC, Uingereza kuhamishia wahamiaji Rwanda
Yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini DRC CENI kusisitiza kuwa uchaguzi utafanyika desemba 20 kama ulivyopangwa; wakati huo huo aliyekuwa mwenyekiti wa CENI Corneille Nangaa alizindua chama kipya cha AFC Alliance Fleuve Congo, wabunge wa Uingereza walipiga kura kuunga mkono mpango wa kuwahamishia wahamiaji nchini Rwanda, siasa za Senegal, na huko Niger Mahakama ya ECOWAS yaamuru kuachiwa huru kiongozi aliepinduliwa nchini Niger Muhamed Bazoum, Jeshi la Israel laendeleza mashambulio mjini Gaza, na pia matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.16/12/202320:15
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.