Jukwaa la Michezo
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Olimpiki: Nigeria na Zambia zafuzu mashindano ya Olimpiki soka ya kina dada
Kwenye makala haya utasikiliza uchambuzi wa mechi za kufuzu soka ya kina dada Olimpiki na shirikisho la riadha duniani kuwa shirikisho la kwanza kutoa tuzo za fedha, maandalizi kuelekea riadha za KipKeino Classic, mkusanyiko wa michezo DRC, uchambuzi wa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Tiger Woods na Novak Djokovic waweka historia kubwa duniani kwenye gofu na tenisi mtawalia.13/04/202423:55 -
CAFCL:Simba na Yanga zabanduliwa michuano ya Klabu Bingwa Afrika
Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchambuzi wa hatua ya robo fainali mkondo wa pili michuano ya Klabu Bingwa Afrika, matokeo ya kufuzu soka Olimpiki ya kina dada, mwanasoka wa Afrika Kusini kuuawa, PSG Academy yatoa mafunzo kwa makocha nchini Rwanda, Kenya yatangaza orodha yake ya wanariadha wa mbio za Marathon kwenye Olimpiki ya mwaka huu, Ufaransa na Kenya kushirikiana kujenga viwanja nane nayo PSG ikiwa tayari kutoa pauni milioni 111 kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen06/04/202423:45 -
WRC Safari Rally Kenya : Mashindano ya mbio za magari yanaendelea nchini Kenya
Karibu katika makala jukwaa la michezo, leo hii tumekuandalia taarifa kadhaa kuanzia katika mashindano ya mbio za magari Safari rally nchini kenya, michuano ya klabu bingwa barani afrika Al Ahly wakiishinda Simba goli moja sifuri kisha Tp Mazembe kupata sare dhidi ya Petro Atletico ya Angola na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Sierra Leone Lamin Bangura afariki akiwa na umri wa miaka 59 katika ajali ya basi.30/03/202423:53 -
Mashindano ya barani Afrika mwaka 2023 yakamilika nchini Ghana
Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na Kenya kuongoza chati ya medali Afrika Mashariki katika mashindano ya Afrika, Shirikisho la soka Cameroon yaondoa kashfa ya udanganyifu wa miaka dhidi ya Nathan Doualla, mkurugenzi mwandalizi wa WRC Safari Rally Jim Kahumbura ajiuzulu, droo ya soka mashindano ya Olimpiki na Nottingham Forest kupokonywa alama nne kutofuata sheria wa fedha Uingereza.23/03/202423:52 -
CAF CL: Tp Mazembe, Yanga na Simba wafahamu wapinzani wao wa robo fainali
Karibu katika makala ya jukwaa la michezo, leo tumekuandalia mengi tukianzia na droo ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani afrika, mashindano ya bara afrika pamoja na droo ya robo fainali katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya.16/03/202423:54 -
Ndondi : Anthony Joshua amshinda Francis Ngannou katika raundi ya pili
Karibu katika makala ya jukwaa la michezo leo tunaangazia kushindwa kwa mwana masumbwi Francis Ngannou na Anthony Joshua,kuanza kwa mashindano ya 13 ya bara Afrika nchini Ghana pamoja na Paris Saint Germain kufuzu katika robo fainali michuano ya klabu bingwa barani ulaya.09/03/202424:04 -
Kenya kujenga uwanja mpya kwa ajili ya michuano ya Afcon mwaka 2027
Karibu katika makala ya jukwaa la michezo leo tunaangazia kujengwa kwa uwanja mpya wa michezo nchini kenya, michuano ya klabu bingwa barani afrika pamoja na taifa la ufaransa kukamilisha ujenzi wa kijiji kitakachotumiwa na wanariadha katika michezo ya olimpiki.02/03/202423:51 -
Mashindano ya Tour du Rwanda mwaka 2024 yamekamilika hii leo jijini Kigali
Karibu katika makala jukwaa la michezo, leo hii tunaangazia kukamilika kwa mashindano ya kuendesha baiskeli ya Tour du Rwanda, mashindano ya mchezo ya gofu Magical kenya open pamoja na klabu ya Yanga na Tp Mazembe kufuzu katika hatua ya robo fainali katika michuano ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani afrika.25/02/202422:41 -
Mashindano ya Tour du Rwanda kuanza hapo kesho katika mji wa Kigali
Karibu katika makala ya Jukwaa la michezo, leo tumekuandalia mengi ikiwemo kuanza kwa mashindano ya kuendesha baiskeli ya Tour du Rwanda, mazungumzo ya kipekee na waziri wa michezo nchini Tanzania Damas Ndumbaro pamoja na kupigwa marufuku mechi nne kwa mchezaji wa timu ya taifa ya senegal Kreppin Diatta.17/02/202424:00 -
AFCON 2024 : DRC kucheza dhidi ya Afrika Kusini katika nafasi ya tatu
Miongoni mwa taarifa kuu tutakazozianhazia ni pamoja na fainali ya kombe la mataifa ya bara afrika AFCON kuchezwa hapo kesho mwenyeji Ivory coast wakipambana na Nigeria. Mchezaji wa tenisi nambari moja barani afrika Ons Jabeur kushindwa katika mashindano ya Abu dhabi na fainali ya kombe la mataifa ya bara Asia kuchezwa leo.10/02/202425:01 -
AFCON 2024: DRC na Nigeria zatinga hatua ya nusu fainali
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na taifa la DR Congo pamoja na Nigeria kufuzu kwa hatua ya nusu fainali katika michuano ya kuwania taji la soka kwa mataifa ya bara Afrika. Dereva wa magari ya langalanga Lewis Hamilton kuhamia katika timu ya Ferrari kutoka Mercedes mwaka 2025.03/02/202423:54 -
AFCON 2024: Michuano ya hatua ya 16 bora kuanza
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya hatua ya 16 kuwania taji la soka kwa mataifa ya bara Afrika. Mashindano ya mchezo wa mikono bara Afrika yanayoendelea kule Misri na Aryna Sabalenka kushinda mashindano ya Australian Open kwa upande wa wanawake.27/01/202423:49 -
Mataifa ya Afrika yaendelea kupambana kutafuta taji la AFCON
Tunaendelea kukuletea uchambuzi wa michuano ya soka kuwania ubingwa kwa mataifa ya Afrika, inayoendelea nchini Cote Dvoire. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania, pia zinapambana kuwania taji hilo. Ungana na wachambuzi wetu Jason Sagini, George Ajowi na Jason Sagini akiwa mjini San Pedro.20/01/202423:56 -
Michuano ya AFCON yaanza nchini Cote Dvoire, nani ataibuka mshindi ?
Michuano ya soka kuwania taji la mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON, inaanza leo nchini Cote Dvoire. Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano haya makubwa kurejea kwenye nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40. Kuna timu 24 zinazotafuta ubingwa wa taji hili, ikiwemo Taifa Stars ya Tanzania na Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Afrika Mashariki na Kati. Wachambuzi wetu Paul Nzioki, George Ajowi na Jason Sagini, akiwa Abidjan, wnachambua.13/01/202423:50 -
CAF yaongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa AFCON 2024
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF kuongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa michuano ya AFCON, itakayoanza Januari 13 nchini Cote Dvoire, Bondia wa DRC Martin Bakole aomba mchango wa fedha kushiriki mechi za mkanda wa WBA, matokeo ya Mapinduzi Cup na kombe la Amani visiwani Zanzibar na Brazil yamfuta kazi kocha Fernando Diniz.06/01/202423:56
Jukwaa la Michezo
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.