Pata taarifa kuu
RWANDA-SANAA-SIASA-USALAMA

Maswali yaibuka kuhusu kifo cha mwimbaji wa Injili Kizito Mihigo

Kizito Mihigo, msanii maarufu wa nyimbi za Injili nchini Rwanda alipatikana amefariki dunia Jumatatu Februari 17 katika chumba ambako alikuwa anazuiliwa kwa muda wa siku tatu jijini Kigali, nchini Rwanda.

Mwimbaji wa maarufu nchini Rwanda Kizito Mihigo aondoka gerezani Nyarugenge, nje kidogo ya Kigali, Septemba 15, 2018.
Mwimbaji wa maarufu nchini Rwanda Kizito Mihigo aondoka gerezani Nyarugenge, nje kidogo ya Kigali, Septemba 15, 2018. Cyril NDEGEYA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Polisi na shirika la upelelezi la Rwanda wanasema alijiua. Lakini baadhi ya watu, wanasema hoja hiyo sio ya kweli.

Mapema Jumatatu wiki hii mamlaka ilitangaza kwamba imeanzisha uchunguzi. Baada ya kutangazwa kifo cha Kizito Mihigo, watu wameendelea kutoa maoni mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mitandao ya Twitter na Facebook, watumiaji wa mitandao wameendelea kunyooshea kidole cha lawama serikali ya Rwanda. "Ni vigumu kuamini kwamba (...) mtetezi wa maridhiano nchini Rwanda hayuko tena katika ulimwengu huu," ameandika Alice Mutimukeye, mmoja wa watumiaji wa mitandao. Kabla ya kuongeza: "Asante kwa mchango wako kwa ujenzi wa Rwanda. Kizito Mihigo pumzika kwa amani.

Pia wanasiasa wa Rwanda wametoa maoni yao. "Watu wenye tabia nzuri hufariki mapema. Ni jambo ambalo halieleweki, "ameandika Victoire Ingabire, mmoja wa wanasiasa wa upinzani, ambaye aliachiliwa huru mwaka mmoja na Kizito Mihigo , 2018, kwa msamaha wa rais Paul Kagame.

 

Baadhi ya watu wameishtumu serikali ya Paul Kagame kwamba ndio ilimuua muimbaji huyo maarufu, ambaye alinusurika katika mauaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.