Pata taarifa kuu
KENYA-DJIBOUTI-AU-UNSC

Kenya yahoji kuendelea kwa Djibouti kutaka kuwa mwakilishi katika Baraza la Usalama

Kenya inahoji kuendelea kwa Djibouti inaendelea kutafuta uungwaji mkono wa kuwa mwakilishi wa bara la Afrika, katika nafasi isiyo ya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, licha ya Nairobi kuungwa mkono na Umoja wa Afrika.

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura.
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura. UN Photo/Loey Felipe
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Raychelle Omamo anatarajiwa kutafuta majibu kuhusu suala hili, wakati wa mkutano mkuu wa 33 wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika, utakaofanyika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia mwishoni mwa wiki hii.

Licha ya Kenya kushinda nafasi hiyo mwaka uliopita, Djibiouti imeendelea kutafuta uungwaji mkono wa kupigiwa kura kutoka kwa mataifa ya Magharibi.

Djibouti inasema licha ya kutokuungwa mkono na Umoja wa Afrika, inataka kiti hico kwa sababu katika historia ya nchi yake, imewahi kuhudumu mara moja tu kati ya mwaka 1993-1994 kinyume na Kenya ambayo imehudumu mara mbili, mwaka 1977-1978 na 1997-1998.

Nairobi inasema inataka Djibouti iachane na harakati zake, kwa sababu haikupigiwa kura na wakuu wa nchi za Afrika, suala ambalo litajadiliwa katika kikao hicho.

Rais Uhuru Kenyatta ambaye yupo ziarani nchini Marekani, hatohudhuria mkutano huo lakini pia anarejea mapema nyumbani baada ya kutokea kwa msiba wa rais wa zamani Daniel Torotich Arap Moi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.