Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Mashauriano yaendelea kuhusu uundwaji wa serikali ya umoja Sudan Kusini

Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Kusini Riek Machar, hatarejea tena jijini Juba wiki hii kuendelea kushauriana na rais Salva Kiir, kuhusu kuundwa kwa serikali ya pamoja, baadaye mwezi huu.

Salva Kiir na Riek Machar walikutana Januari 15 na 16 kujaribu kuendeleza mazungumzo, wakati shinikizo la kimataifa likiendelea.
Salva Kiir na Riek Machar walikutana Januari 15 na 16 kujaribu kuendeleza mazungumzo, wakati shinikizo la kimataifa likiendelea. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Badala yake, Machar na Kiir, watakuwa jijini Addis Ababa, kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Afrika utakaofanyika siku ya Jumamosi.

Katika hatua nyingine, Makamu rais wa Afrika Kusini David Mabuza ambaye ndiye msuluhishi wa viongozi hao wawili yupo Juba, kuendelea na mashauriano zaidi, wakati huu suala la mpangilio wa usalama na idadi ya majimbo likisalia tata.

Machar alikuwa jijini Juba kwa kipindi cha wiki mbili, kufanya mazungumzo na rais Kiir na wadau wengine kuhusu masuala ya idadi ya majimbo na mipaka, na suala la usalama.

Machar na Kiir wameshindwa kuunda serikali mara mbili licha ya kukubaliana, mwezi Mei na Novemba, mwaka 2019 baada ya mkataba wa amani mwaka 2018.

Serikali ya Umoja inatarajiwa kuundwa nchini Sudan Kusini tarehe 22 mwezi huu wa Fbruari, lakini suala tata la kutatua mzozo wa idadi ya majimbo na mipaka yake, huenda likasuburi serikali hiyo kwa mujibu wa wasuluhishi wa mzozo huo ambao ni IGAD na Umoja wa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.